Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Ili kupunguza malalamiko ya Mlundikano wa michango kwa wazazi shuleni Inayosababisha baadhi yao kuitupia lawama serikali Halmashauri ya mji wa Njombe imetenga Fedha kwa ajili ya kusaidia kuwalipa walimu wa kujitolea ambao wamekuwa wakifundisha watoto.
Hatua hiyo imeelezwa wakati Halmashauri ya mji wa Njombe ikipitisha rasimu ya Bajeti ya Zaidi ya bilioni 45.5 kwa Mwaka wa Fedha wa 2025/2026 huku mapato ya ndani yakiwa zaidi ya shilingi bilioni Saba ambapo miongoni Mwa Fedha hizo zitakwenda kulipa baadhi ya walimu hao.
Akiwasilisha Rasimu ya Bajeti hiyo Ofisa Mipango Halmashauri ya mji wa Njombe John Malle amesema pamoja na vipaumbele muhimu katika Bajeti hiyo vikiwemo vya Afya lakini kwenye elimu wameamua kutenga Fedha hiyo iliyoombwa na madiwani kwa miaka mingi.
Baadhi ya madiwani akiwemo Geofrey Mhando na Jactan Mtewele Wamesema Fedha hizo zitakwenda kupunguza mzigo kwa wazazi ambao wamekuwa wakiwalipa walimu hao ambao hawana ajira rasmi kwani itasaidia kuwapa molari ya kufundisha Vizuri watoto.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amewasisitiza madiwani kuwa Fedha hiyo Bado haiwezi kukidhi mahitaji ya walimu wote hivyo suala la kuendelea kuchangia haliwezi kusitishwa huku Katibu tawala wilaya ya Njombe Agatha Mhaiki kwa niaba ya mkuu wa wilaya akipongeza hatua hiyo
0 Comments