Header Ads Widget

WIKI YA MAENDELEO YA JAMII YAADHIMISHWA KWA UFANYAJI USAFI ARUMERU.

Na,Jusline Marco;Arusha

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru kwa kushirikiana na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru TICD kuadhimisha wiki ya maendeleo ya jamii na ubunifu kwa kufanya usafi katika soko la Tengeru Wilayani humo.


Wiki ya Maendeleo ya jamii na ubunifu imefanyika hii leo ikiwa ni kuelekea katika sherehe za Maafali ya 14 ambapo sambamba na ufanywaji wa usafi katika soko hilo, wananchi wamepata nafasi ya kupima afya zao, kuchangia damu na kupatiwa elimu ya utunzaji wa mazingira.





Akizungumza baada ya kumalizika kwa zoezi hilo Afisa Mazingira Halmashauri ya Meru Sai Manyanda amesema lengo la zoezi hilo ni kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali ambazo zinakwenda kutekelezwa.


Aidha ameushukuru uongozi wa chuo hicho kwa utoaji wa vitendea kazi ambavyo vitasaidia katika kuhakikisha suala la usafi wa mazingira  linazingatiwa nadani na nje ya soko hilo na unakuwa endelevu.



Ameongeza kuwa halmashauri ya meru katika kufanikisha hilo inayo mikakati mbalimbali ya kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuweza kuunganisha nguvu ya pamoja katika kuhamasisha wanajamii pamoja na wananchi kwa ujumla kushiruki kwenye usafi wa mazingira.


Awali akizungumza katika zoezi hilo Makamu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii TICD idara ya Fedha na Utawala Janeth Zemba amesema kupitia kaulimbiu ya wiki ya maendeleo ya jamii,kila mmoja analo jukumu la msingi kuielimisha jamii na kufanya usafi kwa vitendo pamoja na kuhifadhi mazingira kwa kizazicha sasa na baadae.

Ameongeza kwa kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika utunzaji wa mazingira kwa kuepuka ukataji wa miti na utupaji wa taka hovyo.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Afisa Tarafa ya King'ori Farhat Juma amesema katika Wilaya ya Meru suala la usafi bado lina muamko mdogo hivyo kama Wilaya wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi kadri wawezavyo  ili wananchi wote waweze kujua mazingira ni afya yao na suala la usafi halikwepeki.


Bi.Farhat amesema mazingira ya kuridhisha katika soko la Tengeru yanatokana na elimu ambayo Halmashauri imekuwa ikiitoa kwa wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo lengo ni kuhakikisha usafi katika Wilaya hiyo unakuwa namba moja.


Ameongeza kuwa kuwataka wananchi kutotupa takataka katika maeneo ambayo hayatakiwa bali wazingatie usafi na kuziweka taka kwenye maeneo sahihi ambapo ametoa rai kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kuungana kwa pamoja kutokomeza uchafu wa mazingira.



Naye Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii TICD Dkt. Anande Kweka amesema kuwa zoezi la ufanyaji usafi katika soko hilo ni sehemu ya kazi zao ya kushirikisha jamii ili kuweza kuwa na maendeleo endelevu ambapo amesema zoezi hilo hufanyika kila mwaka ikiwa ni utaratibu wa Taasisi hiyo kuwa na Juma la maendeleo ya jamii pamoja na ubunifu.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara katika soko la Tengeru Raymond Mkude ameishuku Halmashauri ya Meru pamona naTaasisi ya Maendeleo ya jamii Tengeru kwa kuwakabidhi vifaa hivyo vya kufanyia usafi na kuahidi kuvitumia katika kusudi lililokusudiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI