Header Ads Widget

MWANAHABARI SHALOM ROBERT ASIMIKWA UCHIFU KIJIJINI KWAKE

 




Katika hali ya kushangaza watu wengi hasa kuwahi kutokea kwa kijana mwenye umri mdogo UMOJA wa Wazee wa Mila za asili kutoka Kijiji Cha Kilosa Kata ya Ihanu Wilaya ya Mufindi, wamempokea Mwanahabari Shalom Rober na kumpa heshima ya asili kwa kumuita Chifu KEKOVANGU jina linalomaanisha "Mkombozi wetu".


Hayo yote yamejiri katika Kijiji Cha Kilosa wakati mwanahabari huyo alipofanya ziara ya matembezi.



"Kijana sisi Wazee kwa Umoja wetu tunakusimika Leo pamoja na kukupa jina la Chifu KEKOVANGU lenye maana ya Mkombozi wetu, tunakuombea mafanikio makubwa zaidi hapo baadae". Alisema Kiongozi wa Wazee hao Mzee Ericko Mihale.


Mbali na mambo mengine, Wazee hao wameguswa na ziara ya Mwanahabari Shalom Robert katika Kijiji hicho na kumshukuru kwa mchango wake mkubwa katika kuhamasisha Maendeleo  Kwa Vijana kupitia michezo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI