Header Ads Widget

WAZIRI,DKT BITEKO ANATALAJIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA IJUKA OMUKA KAGERA.

Na Shemsa Mussa -Matukio Daima Blog

                           Kagera

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Biteko anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Tamasha la IJUKA OMUKA litakalofanyika ndani ya Mkoa kagera.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoani humo Mkuu wa Mkoa huo Mhe Hajjat Fatma Mwassa amesema kuwa Tamasha Hilo litazinduliwa rasmi December 18 ambapo itaanza dua kwa ajili ya kuuombea Mkoa kagera, Taifa na kumuombea Rais wa jamhuli ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Aidha Hajjat Fatma amesema,katika Tamasha Hilo zimetengwa siku kumi kwa ajili ya maonesho ya Biashara yatakayofanyika katika viwanja vya ccm ndani ya manispaa ya Bukoba ikiwa lengo ni kuhamasisha wananchi kujitika takita Biashara na kuzitambua fursa zilizopo.

Pia ameendelea kusema kuwa Tamasha la IJUKA OMUKA ni Tamasha la pili tangu kuanzishwa kwake Mwaka Jana na kusema kwa mwaka Jana halikuwaeza kushirikisha watu wengi hivo mwaka huu wataweza kushiriki hasa wananchi wazawa wa Mkoa huo.

"(IJUKA OMUKA) ni neno la kuhaya linalo maanisha kumbuka nyumbani na hivyo tumelenga wazawa wote kushiriki katika Tamasha hili haijalishi wapo hapa Kagera au wapo nje ya nchi,na mwaka Jana tulifanya Ijuka Omuka japo wachache Wetu ndio tulishiriki ila hii ya mwaka huu itakuwa kiboko sana nawakaribisha watu wote ,amesema Mhe Hajjat Fatma"

Mhe Hajjat Fatma,amesema katika Tamasha la IJUKA OMUKA zitakuwepo tamaduni mbalimbali za kihaya ikiwemo burudani za kihaya,vyakula vya kihaya ikijumuishwa na mapishi tofauti tofauti yanayotokana na asili ya Mkoa kagera,huku akisema lengo ikiwa ni kurudisha tamaduni zilizosahaulika.

Amesema Tamasha Hilo litaweza kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo na kupata nafasi ya kukaa na kujadili kwa pamoja ni kwa namna Gani wataweza kushirikiana ili kuinua uchumi wa Mkoa kagera pamoja na kujadili fursa za uwekezaji.

Hata hivyo Mhe Hajjat Fatma,amewapa kipaumbele wananchi wa Mkoa kagera kwa kuwepo matukio tofauti tofauti ndani ya siku nne ili Kila mwananchi aweze kuburudika kwa manma yake ikiwemo Muziki wa taarabu ambapo nayeye atakuwa mshiriki.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI