Header Ads Widget

WADAU SONGWE WAKUTANA KUTAFUTA MUAROBANI VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

 

Na Moses Ng'wat, Songwe.

WADAU kutoka makundi mbalimbali na serikali Mkoani Songwe wamekutana katika mdahalo wa pamoja kwa lengo la kujadili na kujengeana uelewa kuhusu dhana halisi ya ukatili wa kijinsia na madhara yake katika jamii, ikiwa ni pamoja na kupata uzoefu kutoka katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Mkoa huo.

Mdahalo huo ambao umefanyika leo Disemba 6, 2024 na kuhudhuliwa na wadau kutoka makundi mbalimbali, viongozi wa Dini na Mila, Asasi za kirai, Viongozi wa polisi na kusimamiwa na mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, John Mwaijulu. 

Akifungua mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa  ofisi ya Mkuu wa Mkoa zilizopo eneo la Nselewa, Wilayani Mbozi, ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Mwakilishi huyo wa Katibu Tawala , amesema sanjari na suala la ukatili wa kijinsia, pia mdahalo huo  unatoa fursa ya kujadili changamoto ya mimba katika umri mdogo, hasa ikizingatiwa kuwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ndiyo inayoongoza kwa kuwa na changamoto kubwa ya mimba katika umri mdogo na Mkoa wa Songwe ndio ukiwa kinara kwa 45%.

"Matarajio yetu kama mkoa ni kuona washiriki wote  mlioalikwa mnatoa michango Chanya inayolenga kusukuma mbele jitihada za kukabiliana na ukatili wa kijinsia na mimba katika umri mdogo". Alisema Mwakilishi wa RAS.


Mkurugenzi wa jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Badru Abdununi, akitoa takwimu za ndoa na m8mba za utotoni katika mdahalo huo,   zinaonesha kuwa mikoa ya nyanda za juu kusini ya Songwe, Ruvuma, Katavi na Rukwa ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza nchini kwa ndoa na mimba za utotoni, ukiacha mkoa wa Mara ambao uko nje ya kanda ya nnyanda za juu kusini.

Abdununi amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2023, Mkoa wa Songwe ndio unaongoza ukiwa na asilimia 45, ukifuatiwa na Mkoa wa   Ruvuma wenye  asilimia 37 ambapo Mkoa wa Katavi ni wa tatu ukiwa na asilimia 34, wakati Mkoa wa Rukwa wenyewe ukishika nafasi ya tano ukiwa na asilimia 30, huku Mkoa wa Mara ukiwa ni wa nne kwa asilimia 30.

Hata hivyo, kwenye mijadala ndani ya mdahalo huo mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imeonesha kuendelea kuwa vinara wa vitendo vya ukatili wa jinsia katika eneo la ndoa na mimba za utotoni, licha serikali na  wadau wengine kuwekeza nguvu kubwa katika vita hiyo, huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kukosekana kwa malezi bora ya familia.

Miongoni mwa wadau waliochangia katika mdahalo ni Mwenyekiti wa Baraza la ushauri la wazee Mkoa wa Songwe, David Songolo, ametaja miongoni mwa mambo yanayochangia ukatili huo wa ndoa na mimba za utotoni kuwa ni malezi mabovu ya familia.

Songolo amebainisha  kuwa wanaume wengi katika mkoa wa Songwe na ile ya jirani wamekuwa wakiendekeza tabia na mila za kuoa wake wengi  jambo linalichangia malezi mabaya.

Songolo, amesema mila na desturi ya kuwa na wake wengi huwa haiendani na uchumi wa familia hivyo kusababishakukidhi mahitaji ya familia na kusababisha  watoto kukosa ulinzi na kujikuta wakiangukia kwenye vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Hata hivyo, Songolo amependekeza marekebisho ya sheria na kutaka sheria kuwatambua wazee na viongozi wa mila kuwa sehemu katika kusimamia malezi na maadili ya kitanzia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI