Header Ads Widget

VITI 256 VIMENG'OLEWA UWANJA WA MKAPA VURUGU ZA MASHABIKI WA SIMBA NA CS SFAXIEN

 


TAZAMA FULL VIDEO YA VURUGU BOFYA LINK HII

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imesema jumla ya viti 256 vimeng'olewa  katika Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya vurugu kutokea katika mechi ya Simba dhidi ya CS Sfaxien.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro leo Jumapili Desemba 15, 2024 baada ya mechi hiyo.

"kulitokea fujo iliyosababishwa na mashabiki wa Timu ya CS SFAXIEN kutoridhika na maamuzi ya refa wa mchezo huo kuchezesha mechi hiyo kwa zaidi ya dakika saba ambazo aliziongeza kama dakika za nyongeza jambo lililopelekea timu ya Simba kupata goli la pili na la ushindi. Wachezaji wa ndani ya uwanja na "benchi" la ufundi la timu ya CS SFAXIEN walikasirika, wakamfuata mwamuzi wa mchezo na kuanza kufanya vitendo vya kumshambulia.


"Katika fujo hizo shabiki mmoja wa timu ya CS SFAXIEN aliumia na kupatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa, huku viti vya rangi ya blue 156 na Orange 100 viling'olewa na mashabiki hao," imesema taarifa hiyo ya Polisi.

Aidha, imeongeza kuwa Jeshi la Polisi litashirikiana na mamlaka zingine za kisheria na soka kuona hatua za kuchukua dhidi ya vitendo hivyo ambavyo havikubaliki.

Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ilimalizika kwa Simba kuichapa CS Sfaxien mabao 2-1.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI