Header Ads Widget

ANAYEDAIWA KUPOTEA BAADA YA HARUSI ANA MADENI MENGI -POLISI

 


Jeshi la Polisi nchini limetolea ufafanuzi taarifa za Vincent Peter Massawe, ambaye alipotea siku mbili tu baada ya harusi yake na kusema ni kweli kwamba taarifa za kupotea kwake zilifikishwa kituo cha polisi Kigamboni tarehe 19.11.2024 na mke wake na upelelezi ulianza mara moja na kuthibitisha kuwa ni kweli alikuwa na harusi tarehe 16.11.2024 na baada ya harusi alitafuta gari la kuwarejesha ndugu zake na wageni wengine Moshi mkoani Kilimanjaro.


Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime, imeongeza kuwa ushahidi mwingine uliopatikana ni kuwa, wakati wa maandalizi aliazima gari kutoka kwa jamaa yake ili imsaidie katika shughuli za harusi yenye namba T.642 EGU aina ya Toyota Ractis na baada ya harusi hakurejesha gari hiyo kwa mwenyewe, badala yake tarehe 18.11.2024 ambayo inadaiwa alikuwa anafuatiliwa na gari ambayo alikuwa anaitilia mashaka ndiyo siku hiyohiyo aliuza gari hiyo kwa kiasi cha shilingi milioni tisa akalipwa shilingi milioni nane ikabaki milioni moja. 


"Taarifa iliyopo inaonyesha kuwa siku hiyohiyo alimtumia mke wake kiasi cha fedha ili alipe madeni mengine yaliyotokana na harusi ikiwepo coaster aliyokodisha kuwarejesha wageni wake Moshi, gari hilo aina ya Toyota Ractis limefuatiliwa na limekamtwa," imeeleza taarifa ya DCP Misime


Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "ushahidi mwingine unaonyesha huyu Vincent Peter Massawe, pia anadaiwa na watu wengine wawili mmoja kiasi cha shilingi milioni 53, na mwingine shilingi milioni 16, ukweli wa tukio hili utafahamika muda si mrefu kama amejipoteza au la kulingana na mtiririko wa ushahidi ulivyo na hili linategemea hasa tukipata ukweli kutokà kwa mke wake kwani inadaiwa anao ufahamu mkubwa wa jambo hili," imeeleza taarifa ya DCP Misime



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI