Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati Mkoa wa Mbeya Ukiripotiwa kuwapo kwa mlipuko wa Kipindupindu mkoani Njombe Wananchi wametakiwa kuongeza nguvu katika usafi wa mazingira Ili kukabiliana na Janga hilo.
Tayari wameripotiwa baadhi ya wananchi kupatwa na Kipindupindu katika mkoa Jirani wa Mbeya Huku Kata ya Njombe mjini ikiwa na utaratibu wa mara kwa mara wa kuendesha kampeni ya usafi ambapo safari hii kampeni hiyo ilizinduliwa Disemba 9 mwaka huu.
Daina Mgeni ni Ofisa muuguzi Msaidizi Zahanati ya Kambarage wakati wa kuhitimisha Kampeni hiyo anasema ni lazima kuchukua hatua stahiki za kufanya usafi kwani bila hivyo Kipindupindu kinaweza kuwakumba.
Naye Ofisa Afya Halmashauri ya mji wa Njombe Simon Ngasa anasema zoezi la usafi linapaswa kuendelea kila siku ikiwa ni pamoja na kuweka maji ya moto ya kunawa mikono na sabuni ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
Ofisa mtendaji Kata ya Njombe mjini Enosy Lupimo Anawaagiza maofisa Watendaji wa mitaa kuwatoza faini ya elfu 50 wale wote ambao hawajashiriki usafi kupitia kampeni hiyo kwani ni kwa mujibu wa Sheria.
Lupimo amesema zaidi ya Shilingi laki sita zimepatikana kwa kupiga faini waliokaidi kushiriki kufanya usafi kupitia kampeni hiyo na risiti za mashine zimetolewa.
Wananchi wa Mtaa wa Kambarage wanasema wameshiriki kufanya usafi huo ili kuepukana na magonjwa hayo Yanayoweza kuwaingiza kwenye gharama zisizo za lazima.
Disemba 9 mwaka huu Siku ya Uhuru wa Tanganyika Kata ya Njombe mjini Ilizindua Rasmi Kampeni ya Usafi katika Mitaa yote 9 huku wananchi wakishiriki kikamilifu kufanya usafi.
0 Comments