MWENYEKITI wa Chama Cha Mpira wa Miguu wilaya ya Morogoro MMFA Bwana Selestine Mbilinyi amesimamishwa Uongozi baada ya kutuhumiwa kuingiza siasa katika majukumu yake ya kuongoza soka.
Uamuzi wa kumsimamisha upngoziy Mwenyekiti huyo umefanywa na Uongozi wa Kamati tendaji ya Chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro MRFA baada ya kupokea barua ya malalamiko kutoka kwa Mbunge wa Morogoro Mjini Bwana Abdul- Aziz Abood.
Akitangaza uamuzi huo baada ya kikao cha kamati tendaji, Mwenyekiti wa MRFA Paschal Kihanga amesema hatua hiyo imekuja baada ya Mwenyekiti huyo kumpa nafasi ya kudhamini ligi daraja la nne kiongozi mmoja wa kisiasa, aliyewahi pia kugombea ubunge Jimbo la Morogoro Mjini na kutoa pia jezi zenye jina lake kwa madai kiongozi huyo ameingia maktaba na MMFA.
Kihanga akasema baada ya kupokea barua hiyo ya malalamiko kutoka kwa Mbunge Abood ikieleza malalamiko kuwa Mwenyekiti huyo amekuwa akiigiza siasa katika michezo, kamati hiyo ililazimika kukutana pamoja na kufikia uamzi huo baada ya mwenyekiti huyo kukiri mbele ya kamati hiyo kufanya hivyo bila kujua kuwa ni kosa.
Mwenyekiti huyo akawataka viongozi wa vyama vya siasa mkoani Morogoro kuzingatia kanuni na miongozo ya Shirikisho la chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Akasema kitendo cha kuchanganya siasa na mpira kumesababisha pia mkoa wa Morogoro kufungiwa kwenye masuala mbalimbali ya kisoka.
Mwisho
0 Comments