Na WILLIAM PAUL , SAME.
KAMPUNI inayotoa huduma za usafirishaji wa mizigo na uwakala wa forodha (Mwembe logistics) imeendelea kufanya vizuri na kuwa wabunifu zaidi Katika utoaji wa huduma zake.
Akizungumza kwenye tamasha la utalii wilayani Same lijulikanalo kama Same utalii festival season two meneja Mkuu wa mwembe logistics James Tindi amesema wameendelea kujipambanua na kuongeza ubunifu katika utoaji wa huduma zake kwa wateja wao.
James amesema wameendelea kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya usafirishaji wa mizigo na awamu hii wamepanua wigo na kuwekeza katika utalii hivyo wataendelea kuwafikia watu wengi zaidi kwenye huduma yao huku akisema yote hayo ni kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika kutangaza vivutio vya utalii Nchini.
"Sisi kama kampuni inayotoa huduma za usafirishaji tumeendelea kuongeza nguvu katika kutoa huduma zetu kwa wateja wetu na sasa tumejikita pia katika kusafisha mizigo mbalimbali ndani na nje ya Nchi ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za kutangaza utalii wa Tanzania pia tumekuwa tukishiriki kwenye matamasha mbili hivi ya utalii kama sehemu ya huduma zetu" Alisema James meneja wa mwembe logistics".
Aidha akiwa wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kwenye uzinduzi wa tamasha la Same utalii festival season two Waziri wa Mali asili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana amewapongeza kampuni ya Mwembe logistics kwakuendelea kuwa wabunifu zaidi katika utoaji wa huduma zake huku akiendelea kuwasihi kuendelea kuongeza nguvu zaidi na ubunifu kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya Nchi katika utoaji wa huduma zake.
Mwisho.
0 Comments