Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Daud Yassin (Kushoto) akimkabidhi tuzo ya shukrani mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC)Salim Abri Asas kwa kukusaidia Chama hicho kupata ushindi wa asilimia 99.99 kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27 mwaka huu picha na Matukio Daima media
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Halmashauri Kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa imempa tuzo ya shukrani Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Salim Abri Asas, kutokana na kuwa na mchango mkubwa ndani ya chama hicho.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi (CCM)mkoa wa Iringa, Daudi Yasin wakati wa kikao Cha Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Iringa jana .
Yassin alisema kuwa chama cha mapinduzi kinatambua juhudi kubwa zinzofanywa na MNEC, Asas katika kuimarisha na kuendeleza chama hicho.Amesisitiza kuwa MNEC, Salim Abri Asas amekuwa msaada mkubwa wa kipekee kwa chama hicho, kwa kutoa mchango wa hali na mali ili kuhakikisha chama kinaendelea kutimiza majukumu na malengo yake.
“Tuzo hii ni ishara ya kutambua na kuthamini juhudi zako MNEC Asas ambazo zimekuwa ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya ccm, alisema Daudi Yassin.
Aidha, baada ya kupokea tuzo hiyo, MNEC Salim Abri Asas amewashukuru viongozi na wajumbe wa CCM Mkoa wa Iringa kwa kutambua mchango wake huku akiahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za chama katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mnec Asas ameahidi kuwa atazidi kuimarisha na kudumisha uhusiano wa karibu kati yake, chama na wananchi, huku akiwapongeza wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kuendelea kuwa na imani na CCM.
Katika hatua nyingine, MNEC Asas alitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, akimpongeza kwa mchango wake mkubwa ndani ya CCM na taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa Rais Samia ameonyesha uongozi bora ambao umeleta mabadiliko chanya katika nchi, ambayo yanajuhudi za kujenga taifa.
0 Comments