Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Hassan Rugwa (kushoto) akipokea majiko mawili ya kupikia yanayotumia umeme yaliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda (UNIDO) kwa shule ya sekondari ya wasichana Kigoma iliyopo Uvinza mkoani Kigoma anayekabidhi majiko hayo ni Mwakilishi wa UNIDO Doroth Kitutu (kulia).
Na Fadhili Abdallah, Kigoma
shirika la umoja wa mataifa la maendeleo ya viwanda (UNIDO) limekabidhi majiko mawili ya umeme ya kupikia kwa shule ya Sekondari Wasichana Kigoma wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
mwakilishi wa UNIDO, Doroth Kitutu alikabidhi majiko hayo kwa Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Hassan Ruga kwa niaba ya shule hiyo ambapo UNIDO inasema kuwa imetoa majiko hayo kuunga mkono azimio la Raisi Samia Suluhu Hassan la matumizi ya nishati safi.
Afisa elimu wa mkoa Kigoma Pauline NdigezeUNIDO imesema kuwa majiko hayo mawili ambayo yanagharimu jumla ya shilingi milioni 14 yametolewa kupitia mradi wa pamoja Kigoma (KjP) na kwamba wametekeleza ombi lililowashilishwa kwenye kikao cha kamati ya utendaji wa mradi huo na kwamba wataendelea kusaidia kutoa fedha kwenye shule nyingine kadri uwezo utakavyoruhusu.
Akizungumza wakati akipokea majiko hayo Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Hassan Rugwa ameishukuru UNIDO kwa msaada huo ambao kwa kiasi kikubwa unazingatia matumizi ya majiko ya kupikia yanayozingatia uhifadhi wa mazingira
Mwakilishi wa UNIDO Doroth KitutuKwa upande wake Afisa elimu wa mkoa Kigoma Pauline Ndigeze alisema kuwa tayari shule hiyo mpya ya wasichana ya mchepuo wa sayansi ya bweni imeshaanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano kuanzia mwezi julai mwaka huu na mwezi januari shule itapokea wanafunzi wengine 120 wa kidato cha kwanza.
Ndigeze alisema kuwa kutolewa kwa majiko hayo kunaunga mkono mpango wa serikali wa matumizi ya nishati safi kwenye shule za bweni ikiwa ni kutunza na kuhifadhi mazingira ili yasiharibiwe na matumizi ya majiko ya kuni ya kupikia
0 Comments