Mdau wa maendeleo ya vijana na mwanahabari Shalom Robert, ametembelea vijiwe vya boda boda wilayani Mafinga, mkoani Iringa, na kuzungumza na vijana kuhusu umuhimu wa mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na serikali kupitia halmashauri.
Akizungumza na vijana hao, Shalom amesema kuwa ametembelea kundi hilo la vijana wa boda boda kutokana na kuonekana kusahaulika, licha ya kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa serikali inatambua juhudi za vijana hao na ndiyo maana inaendelea kuwawekea mazingira wezeshi zaidi ili waendelee kuchangia maendeleo yao binafi na ya taifa.
Katika hatua nyingine, Shalom amepongeza kazi nzuri zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, na kusema kuwa vijana wanaona na kutambua juhudi hizo.
Aidha ameelezea furaha yake kutokana na hatua zinazochukuliwa na serikali ya kuleta maendeleo, hasa kwa kuwapa vijana fursa mbali mbali za kufaidika ikiwemo mikopo isiyokuwa na riba, ambayo ni moja ya juhudi muhimu za kuhakikisha ustawi wa kundi hili muhimu la kijamii.
0 Comments