Header Ads Widget

MBOWE ATANGAZA KUCHUANA NA LISSU UENYEKITI

 



Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) taifa, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kuwa atagombea tena, nafasi ya uenyekiti ndani ya Chama hicho ili kutetea kiti chake na kuchuana na viongozi wengine ambao watagombea nafasi hiyo akiwemo Makamu mwenyekiti wa chama hicho,Tundu Lissu.

Akiongea na Wahariri Jijini Dar es salaam leo, Mbowe amesema kuwa ametafakari kwa kina jambo hilo na kufanya maamuzi hayo ambayo alikuwa akipokea maoni mengi kutokwa kwa watu tofauti. 


Mbowe amesema alishawahi kutangaza mara nyingi, kuwa anatamani kuachia nafasi hiyo lakini ni mpaka muda utakapo fika.


“Nimetafakari kwa kina sana, nimesema mara nyingi nilitamani kuondoka lakini siwezi kuondoka na minyukano ambayo ipo ndani ya Chama , kwahiyo CHADEMA nipo, nitakuwepo, nitagombea na Mimi na Viongozi wenzangu wanaoniunga mkono na wasioniunga mkono naamini tutakutana kwenye mazungumzo tuweke mambo sawa, sijawahi kuzuia Watu kugombea, anayetaka kugombea tukutane kwenye box”

“Wazee walioasisi Chama chetu hawakuondoka madarakani kwakuwa walitaka kung’atuka, waliamua kuondoka kwasababu walikuwa wametimiza wajibu wao mkubwa wa kujenga Chama imara chenye itikadi na sera madhubuti, tukumbuke Mzee Edwin Mtei Mwenyekiti wa kwanza wa Chama aliondoka akiwa na umri wa miaka 68, miaka mitano baadaye Mzee Bob Makani Mwenyekiti wa pili yeye aliondoka akiwa na miaka 67, wote waliondoka sio kwasababu ya kushindwa bali kwakuwa walikuwa wamemaliza kazi zao za kuimarisha sera”

“Nilipokea kijiti cha kuongoza Chama chetu September 14,2004, katika miaka hiyo 20 ni kipindi cha miaka 11 tu ya kwanza ambapo tulifanya kazi kikamilifu ya kujitoa ili kukijenga Chama chetu kuwa Chama makini na tukapiga mafanikio ya kufanya tuwe Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania”

“Tumefanya mambo mengi ikiwemo kubuni vazi maarufu la Chama maarufu kama kombati na kuongeza thamani ya Chama chetu kwa kuvuta Wanasiasa makini kutoka Vyama vyote na Vyuoni hadi Watu wakafananisha Chama na Real Madrid ambayo inaweza kuvuta Mastaa kutoka Timu mbalimbali, tukapata wengi Mastaa waliokuja kuongeza thamani ya Chama chetu”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI