Madereva wa Bodaboda na wale wa Bajaj katika jimbo la Uyole mkoani Mbeya wameeleza kumuunga mkono mwenyekiti wa UVCCM Mbeya mjini anayegombea udiwani kata ya Nsalaga wakisema ni kijana makini kuwaunganisha wananchi wakiwemo vijana.
Wamesema hayo kwa nyakati tofauti kwenye hafla ya mgombea huyo kuchukua fomu ya kugombea udiwani kata ya Nsalaga jimbo jipya la Uyole ambapo wamesema Clemence James Mwandemba amekuwa na ushirikiano na wana jamii na kuwa mshawishi wa maendeleo hivyo wanaamini atafaa kuwa mwakilishi wa wananchi katika baraza la madiwani na kutatua kero zao.
Akizungumza mbele ya wanachama na viongozi wa CCM kata ya Nsalaga, Mwandemba ameahidi kuendelea kuwa mwaminifu katika kuwatumikia wananchi wote bila kujali makundi na tofauti zao za kisiasa wala kiimani.
Amekishukuru chama chake kwa kumuamini kuwa atafaa kuwa Diwani wa kata ya Nsalaga na kuwataka wana-chama wenzake kuvunja makundi baada ya uchaguzi wa ndani kukamilika badala yake waungane kwenda kutafuta kura kuelekea uchaguzi mkuu baadaye Oktoba 29, 2025 kuhakikisha CCM inashinda.
0 Comments