Header Ads Widget

MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN KUZINDULIWA MOROGORO

Na Lilian Kasenene, Morogoro

Matukio DaimaApp 

MKUU wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala amewataka wananchi wa mkoa wa Morogoro kutumia fursa ya kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia 'Mama Samia Legal Aid Campaign' katika kutatua changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili wananchi wanyonge wakiwemo wanawake na watoto.

Aidha amesema kampeni hiyo itasaidia upatikanaji wa mifumo ya utoaji haki, na masuala ya kisheria kwa wananchi.

Alisema hayo mjini Morogoro wakati akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya uzinduzi wa kampeni hiyo inayotarajia kuanza Disemba 13.

Kilakala alisema kampeni hiyo inalenga kulinda na kukuza haki ya upatikanaji haki kupitia huduma za msaada wa kisheria nchini na kwamba itachangia kuimarisha Amani na utulivu, kuongeza kipato Cha mtu mmoja mmoja na kuleta utengamano wa kitaifa.

"Nitoke wito kwa wananchi wote katika mkoa huu wa Morogoro fursa hii adimu kushiriki na hatimaye kupata elimu ya msaada wa kisheria na kuzitatua kero na migogoro yao bila malipo yoyote,"alisema DC Kilakala.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema mara baada ya kuzinduliwa utekelezaji wake utaendelea katika ngazi za Halmashauri ambapo wataalamu watafika kwenye kata na vijiji/mitaa.

Alisema lengo lingine ni kukamilisha ndoto za Rais Samia Suluhu Hassan za kutaka kuwapatia haki ya msingi wananchi walio wanyonge.

Kampeni hiyo ya kisheria inatekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya katiba na Sheria na inalenga pia kuongeza uelewa wa kisheria na upatikanaji wa haki na haki za binadamu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI