Header Ads Widget

WENYEVITI WA MITAA,VIJIJI,VITONGOJI NA WAJUMBE WALA KIAPO NJOMBE


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Ikiwa imepita siku moja baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa tayari viongozi waliochaguliwa wameshakula Kiapo tayari kwa kazi ya kuwatumikia wananchi.

Mkoani Njombe baadhi ya kata zimesha apisha viongozi hao ambapo Hakimu wa Wilaya ya Njombe Izack Romanus Mlowe wakati akiwaapisha wenyeviti wa mitaa mbalimbali Katika Halmashauri ya mji wa Njombe amesema kiapo hicho kinawataka kwenda kuwatumikia wananchi kwa weledi mkubwa na kwa kufuata sheria.



Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Kuruthum Sadick amewapongeza wenyeviti hao kwa ushindi na kuwataka kwenda kuwatumikia wananchi kama yalivyo matarajio yao.


Baadhi ya Wenyeviti wa mitaa na Wajumbe akiwemo Subira Kyando,Francis Msanga na Rehema Mwogofi wameahidi kwenda kufanyakazi ya kuwatumikia wananchi kwa weledi mkubwa na kukamilisha miradi iliyopo.


Kwa upande wao wananchi Mkoani Njombe akiwemo Kipson Mtweve na Neema Mahenge wamewataka viongozi hao kwenda kufanyakazi mara mbili ya kazi zilizofanyika kipindi kilichopita kwani wana matarajio makubwa.

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amesema zoezi la Uchaguzi lilikwenda vizuri na kwa ambaye hajaridhishwa na Matokeo anapaswa kufuata sheria na sio Kufanya Vurugu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI