Header Ads Widget

CHADEMA KUKUTANA KWA KIKAO CHA DHARURA IJUMAA HII

 


SAKATA la rafu za Uchaguzi wa serikali za mitaa laikutanisha kamati Kuu ya CHADEMA ambayo imepanga kukutana katika kikao maalum cha dharura kesho Ijumaa November 29,2024 ambako kikao hicho kitajadili ajenda maalum ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.


Taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo imesema “Kikao hicho kitakachojadili agenda maalum, yaliyojiri kwenye kinachoitwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Viongozi 2024 na hatimaye kutoka na msimamo wa Chama, kikao hicho kitakaongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, kauli rasmi ya Chama itatolewa baada ya kikao hicho kumalizika” 


CHADEMA ilisema Wanachama wake watatu katika Mikoa mitatu tofauti wameuawa kikatili katika matukio ya kukatwakatwa mapanga pamoja na kupigwa risasi, Wanachama hao ni Steven Chalamila wa Jimbo la Tunduma ambaye alivamiwa na kukatwakatwa mapanga kikatili hadi umauti kumkuta huku Mgombea nafasi ya ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ulongoni A Kata ya Gongo la Mboto, Ukonga Dar es salaam aitwae Modestus G. Timbisimilwa amefariki baada ya kupata kipigo

kutoka kwa Askari Polisi alipokuwa anazuia kura feki kuingizwa kwenye masanduku ya kura leo mchana.


Taarifa hiyo ilieleza kuwa Mwanachama mwingine aitwae George Juma Mohammed wa Kitongoji cha Stand Kata ya Mkwese Jimbo la Manyoni Mkoani Singida alivamiwa nyumbani kwake na Watu waliojitambulisha kuwa Askari Polisi na kumpiga risasi iliyomsababishia umauti huku tukio jingine la Katibu wa Chama Wilaya ya Singida Mjini Hamis Nkua akichomwa kisu begani, baadaye Jeshi la Polisi katika taarifa yake ilitoa ufafanuzi wa taarifa kuhusu kifo cha Modestus G Timbisimilwa ambaye alikuwa Mgombea Ujumbe Mchanganyiko wa

Mtaa na Wakala wa Nje wa CHADEMA kuwa ameuawa na kutelekezwa na Polisi ambapo limesema taarifa hizo ni za uongo “Taarifa kuhusiana na kifo hicho ni kwamba leo November 27,2024 majira ya saa 2.10 Modestus G Timbisimilwa alifika katika Kituo cha kupigia kura cha Ulongoni A Gongolamboto Jimbo la Ukonga na kuelekea kituo namba 5 akiwa anafuatilia masuala ya uchaguzi”


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI