Na Shemsa Mussa -Matukio daima App
Bukoba,Kagera.
Katika siku ya kihistoria kwa Jimbo la Bukoba Mjini, Mbunge Wakili Stephen Byabato leo, tarehe 27 Novemba 2024, amepiga kura katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa katika kituo cha Chuo Huria, Mtaa wa Migera - Nshambya.
Mbunge Byabato amesisitiza umuhimu wa kila mwananchi kutumia haki yake ya kupiga kura, akisisitiza kwamba ni wajibu wa kila mmoja kuchagua kiongozi anayemfaa.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura, Byabato alieleza kuwa, "Ni haki ya kila mwananchi kumchagua kiongozi anayemtaka.
"Niko hapa kuwakumbusha wananchi ambao hawajapiga kura kuharakisha kufika katika vituo vya kupigia kura ili waweze kupata viongozi wanaowataka" alisema mbunge huyo.
Katika juhudi za kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika uchaguzi huo muhimu, Byabato alitangaza kuanzisha zoezi la hamasa la nyumba kwa nyumba, akisema, "Kupiga kura ni fursa ya miaka mitano, na ikipita, huwezi kuipata tena hivyo nitahakikisha hakuna anaye baki nyuma."
Mbunge huyo pia alitoa shukrani kwa wananchi kwa mwitikio mkubwa aliouona katika vituo vya kupigia kura, akisema, "Nawashukuru wananchi kwa mwitikio mkubwa niliouona wakati nikienda kupiga kura mimi na familia yangu."
Kwa hakika, juhudi za Byabato zinaonyesha dhamira yake ya kuimarisha demokrasia na kuhakikisha kila sauti inasikika katika uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.
Vile vile ,Mbunge wa Viti maalum anayetokana na Asasi za Kiraia Tanzania Bara Neema Lugangira amewaongoza wakati wa mtaaa wa Rwome kata Kashai Manispaa ya Bukoba ambalo ni Jimbo la Bukoba Mjini kupiga kura ya kuwachagua viongozi wa serikali za Mitaa
Akiwa katika kituo Cha kupigia kura shule ya sekondari Kahororo amesema amevutuwa na wingi wa watu waliojitokeza kupiga kura na utaratibu wa wananchi kupiga kura unavyofuatwa.
"Nimeshuhudia shauku na wingi wa watu waliokuja kupiga kura hakika wananchi wameamua kama Kuna watu hawajatoka nyumbani kuja kupiga kura wafike haraka ili kutimiza wajibu na kupata haki ya kuwapata viongozi wao mazingira ni mazuri na hauchelewi"anasema Lugangira
Alitoa shukurani kwa serikali kutoa Fursa ya mapumziko kwani hata wafanyanyazi na wanafunzi waliotimiza umri wote watapata Fursa ya kupiga kura .
0 Comments