Header Ads Widget

RAIS DKT.SAMIA AUPONGEZA MKOA WA ARUSHA KWA UTALII WA MIKUTANO

NA,JUSLINE MARCO;ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Novemba 27 ameupomgeza Mkoa wa Arusha kwa kuwa na mikutano mikutano mingi ambayo inachangia na kukuza sekta ya utalii mbali na maendeleo ya biashara wananchi wamaufanya mkoa huo kuwa salama.


Rais Dkt.Samia ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini na wadau wa utalii katika viwanja vya ndege vya Kimataifa Kilimanjaro KIA ambapo ametoa heshima kwa Mkoa wa Arusha ambao ndiyo makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Vilevile ametumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi kujitoa na kushiriki zoezi la upigaji kura na kuchagua viongozi katika maeneo yao na kuwataka kuendelea kusubiri matokeo katika hali ya usalama na utulivu.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda akizungumza katika Biwanja hivyo kwa niaba ya Wadau wa utalii amemshukuru Rais Dkt.Samia kwa kurejesha uhai wa uchumi katika sekta ya utalii na kuongeza tija kwenye mnyororo mzima wa sekta ya utalii hali iliyochangia wananchi wengine kuweza kupata ajira.


Ameongeza kuwa mwaka 2021 sekta ya utalii ilikuwa na mzunguko wa fedha wa shilingi bilioni 3 peke yake,hivyo kutokana na juhudi za Rais Dkt.Samia za kuifungua nchi kwa kukubali watanzania kuchanjwa hali iliyosababisha mataifa mengi kuanza kuruhusu watalii kutembelea hifadhi nchini.


Makonda ameeleza kiwa mapato ualiyokuwa yatapatikana kutokana na viingilio Tawa,Ngorongoro pamoja na Tanapa kwa mwaka 2021 yalikuwa ni bilioni 125, mwaka 2023/24 mapato yameongezeka hadi kufikia bilioni 801 na ajira kuongezeka kwa kiasi kikubwa upande wa utalii katika Mkoa wa Arisha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI