YAZINDUA MRADI WA USAWA WA KIKODI KWA WAKULIMA
Na Lilian Kasenene,Morogoro
Matukio DaimaApp
Sekta ya kilimo pamoja na kuchangia pato la taifa asilimia 27, imeelezwa kuwa wakulima wengi hasa wa vijijini bado wapo katika mifumo isiyo rasimi inayowafanya kushindwa kushiriki kwa urahisi kwenye suala la ulipaji kodi.
Afisa program kutoka shirika la Pelum Tanzania Anna Marwa alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa Mradi wa Usawa wa Kikodi kwa Wakulima uliofanyika mkoani Morogoro.
Marwa alisema lengo la mradi ni kuonyesha namna wakulima wanavyoweza kushiriki katika masuala ya ulipaji kodi kwa kupatiwa elimu za usawa zinazoweza kunufaisha wanawake na vijana hasa katika maisha yao.
Alisema mradi huo mbali na kuwajengea uelewa katika ulipaji kodi unalenga kuwezesha wanawake kushirika katika michakato mbalimbali ya utungaji wa sera, miongozo na sheria ambayo inaweza kuwasaidia kuanzia ngazi ya jamii hadi kufikia taifa.
“Lakini wao kama wanawake lazima wahamasishane wao kwa wao kwenye suala la ulipaji kodi,lengo ni kuhakikisha wanaboresha maisha yao hasa wanawake na vijana kwani ndilo kundi ambalo lina changamoto nyingi, na ndio makundi yanayochangia maendneleo na masuala mengi ya kilimo,”alisema Marwa.
Aidha alisema pamoja na kwamba wakulima ndio kundi kubwa linalochangia pato la taifa, wengi wao hawana uelewa hasa kwenye maeneo mawili ya Tozo na kodi hivyo wengi wanashindwa kushiriki katika kulipa kodi.
Katika ngazi za vijiji wakulima wengi hawaelewi kuhusu tozo na kodi pamoja na kwenye maeneo yao kuna tozo mbalimbali zilizoanzishwa kama za mazao na malighafi ambazo nyingi wanalipa baada ya mavuno zile zinaanzishwa kwa kulenga kuboresha kitu Fulani.
Kwa mradi huo unajenga uelewa juu ya masuala ya kodi ya usawa na namna wanavyoweza kushiriki kulipa kodi.
Mtaalamu wa masuala ya kodi Samuel Mkwatwa alisema kilimo kina mchango mkubwa hivyo serikali wakati wa mipango yake lazima izingatie watu wenye mahitaji na vipaumbele hasa katika kilimo,kilimo cha Tanzania kwenye maeneo mengi ni wakulima wadogo.
Wakulima wanayo mahitaji mengi kama pembejeo wanatakiwa kufikiwa kila wakati na kutafiti ndogo zisizo lasimi wanawake ndio wamekuwa walipa kodi kwenye maeneo mengi.
Mtaalamu huyo alisema mradi huo unatamani kuona wanawake na vijana wananufaika na kushiriki katika suala zima la ulipaji kodi na hiyo kwa kupata uelewa zaidi.
Akizungumza katika kikao hicho cha kutambulisha shughuli za mradi huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro(Morogoro DC)… alisema kujengewa uwezo kwa wananchi kunasaidia katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao na kuwajengea kujitambua, kumuondoa katika umaskini, ikiwa ni pamoja na kuwaeleza kuwa wanawake na vijana wanastahili kumiliki mali hasa ardhi.
“Siku zote nawaeleza wananchi kwenye Halmashauri hii kuwa mali si kuwa na vitu, bali mali ni ardhi ambayo inaweza kukusaidia katika nyanja mbalimbali kama kupata mkopo kutoka kwenye taasisi za kifedha na nyinginezo,’alisema.
Alisema wananchi walio wengi wamekuwa wamekuwa hawaoni umuhimu na thamani yua ardhi, na kwamba umefika wakati kuendelea kupatiwa elimu na kuthamini ardhi yao.
Mwenyekiti huyo alipongeza kuwepo kwa mradi huo ambao utawezesha wananchi kukua kiuchumi na kusaidia familia, na kutoa ushauri kuwa inatakiwa kuongeza nguvu katika mazao ya viungo vya aina zote kwa kuwapatia miche ya aina zote na kwamba hiyo itasaidia kulindwa kwa uoto wa asili,kusaidia milima kulindwa na kuwepo kwa mashamba darasa yatakayosaidia wananchi kuinuka kiuchumi na kuongeza mbegu za asili huku akitaka kutolewa kwa mafunzo kwa watoa maamuzi.
Mmoja wa wakulima kutoka kijiji cha Kungwe Shani Kibwende alisema suala la kikodi kwao bado imekuwa tatizo lakini baada ya kupata elmu ni imani yake kuwa sasa watakuwa washiriki vyema katika suala zima la ulipaji kodi huku akiomba serikali na Pelum kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili suala zima la kodi liweze kufahamika hasa maeneo ya vijijini.
Mradi wa Usawa wa Kikodi kwa Wakulima ni wa miaka miwili unafanyika katika vijiji vya Kikundi, Kungwe, Lukonde na vuleni vilivyopo kata ya Tomondo wilaya ya Morogoro na unalenga wanawake na vijana.
Mwisho.
0 Comments