Header Ads Widget

BODI YA WAKURUGENZI NCAA YAFANYA UKAGUZI MSOMERA



Na Jusline Marco;Tanga


Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imefanya ukaguzi wa miundombinu mbalimbali katika kijiji cha Msomera Mkoani Tanga.


Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali Venance Mabeyo amewaongoza wakurugenzi hao katika ukaguzi huo ili kuhakikisha wananchi wanaohamia katika kijiji hicho kutoka kwenye Hifadhi ya Ngorongoro wanapata mahitaji yote muhimu ambayo yanahitajika katika maisha ya kila siku.



Aidha ameongeza kwa kuwashukuru watendaji wa Sekta zote katika kijiji cha Msomera kwa ukamilishaji wa nyumba 2500 na miundombinu ambayo ipo kwenye eneo hilo ikiwemo tenki la maji lenye ujazo wa lita laki moja ambapo amesema katika eneo hilo lililokuwa kame limekuwa mkombozi wa wananchi hao na kuweza kuleta matumaini.


"Vilevile tumeona ujenzi wa tenki jingine la lita laki sita na hamsini ambalo nalo liko katika hatua za kuanza kujengwa na hivyo kuleta matumaini kwa wakaxi wa huku msomera ambao wametoka Ngorongoro ili kupisha uhifadhi."Alisema Kanali Venance


Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amewataka wananchi walioko katika hifadhi ya Ngorongoro na ambao wapo tayari kuhamia Msomera kuwa nyumba katika kijiji cha Msomera zipo na zimeshakamilika.



Naye Kaimu Kamanda wa Oparesheni ya Ujenzi wa nyumba hizo Luteni Kanali Edward Mwanga amesema katika jukumu la ujenzi wa nyumba 2500 alilopewa kulisimamia katika kijiji cha msomera tayari nyumba hizo zimekamilika kwa asilimia 100 na kujengwa kwa viwango vya kisasa na ubora jnaotakiwa.


"Kilichoobaki sasa tunadubiri maelekezo kwenda kumalizia nyumba elfu moja zilizoko Saunyi na nyumba elfu moja na mia tano Kitwai B katika Wilaya ya Simanjiro."Alisema 

Luteni Kanali Edward Mwanga



Awali akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro,Kamishna msaidizi Mwandamizi Idara ya Maendeleo ya Jamii) Grolia Bidebeli amesema kuwa kazi yao ni kuhakikisha wanaendelea  kuwahamasisha wananchi ambao bado wapo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro waweze kuhama kwa hiyari yao ambapo wanatarajia kuwaleta katika makazi hayo wananchi ambao tayari wamejiandikisha.


Zoezi la uhamishaji wananchi kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro lilianza Juni 2022 kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi waishio ndani ya hifadhi hiyo nje ya hifadhi ili kupisha na kuimarisha shughuli za uhifadhi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI