Header Ads Widget

KIDULI BAADA YA KUFUZU HATUA YAPILI YA KOMBE LA CRDB YAWASHUKURU WADAU.

 


TIMU ya soka ya Kiduli Football Club ya Wilayani Kibaha imewashukuru wadau mbalimbali kikiwemo Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) na Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) kwa ushirikiano walioutoa na kufanikisha ushindi dhidi ya timu ya Youth ya Morogoro kwa magoli 2-1kwenye mchezo wa kombe la CRDB mchezo uluofanyika Morogoro.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa timu hiyo ya Kiduli Ally Masimike imesema kuwa anatoa shukrani kwa wadau wote waliofanikisha ushindi huo kwani kazi kubwa imefanyika.


Masimike amesema kuwa ushindi huo umewafanya waende hatua ya pili ya mashindano hayo hivyo ni heshima kwa Wilaya ya Kibaha na Mkoa wa Pwani kiujumla.


"Tumefurahishwa na ushirikiano mliouonyesha kupitia vyama vyetu COREFA na KIBAFA kwani hivi ndiyo baba wa vilabu vyetu na mmeonyesha hilo kuwa nyie ni wasimamizi wazuri wa mpira wetu na tunaomba ushirikiano huu uendelee na kwa vilabu vingine,"amesema Masimike.


Aidha ameomba mechi ijayo Vyama vya Soka vya Wilaya  zote zitume wawakilishi ili waweze kujifunza kitu katika michuano hiyo nakuomba ushirikiano huo uendelee kwa vilabu vyote ili Mkoa wa Pwani upige hatua kwenye mashindano mbalimbali.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI