Header Ads Widget

VIJANA WAITWA KUHUDHURIA KONGAMANO LA VIJANA DODOMA

 


Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka Vijana wenye sifa za ujuzi wowote kutoka vyuo mbalimbali hapa Nchini kuhudhuria katika Kongamano la Vijana ili kukutana na wadau na kuangazia fursa mbalimbali zilizoandaliwa na Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau.


 Mkuu huyo ameyasema hayo jijini hapa wakati akizungumza na Wanahabari kuhusu na kongamano hilo litakalo fanyika kwa siku mbili November 19 na 20 ambalo lomeandaliwa na Mkoa na Taasisi ya Mafunzo na Maendeleo ya Vijana(STRATEGIUS ADVISORY) 


Amesema Kongamano la mwaka jana 2023 walipata shuhuda kutoka kwa vijana wengi ambao wamefanikiwa baada ya kupata mafunzo ya kongamano hili kwani walipata kujifunza namna ya kuchangamkia fursa na wapo waliopata Tenda kwenye Serikali kupitia Sheria ya PPRA.


"Na mimi nitoe wito kwa vijana wote wenye sifa au kuhitimu chuo chochote,wana ujuzi wao lakini bado wanatafuta fursa mbalimbali au wale ambao bado wapo chuoni,ni nafasi yao nzuri sasa kuja kutumia fursa iliyoandaliwa na Mkoa wa Dodoma na kushirikiana na wadau ili waweze kufaidika nayo".


Na kuongeza "Mwaka jana tulipofanya lile kongamano tulipata shuhuda za vijana,wapo vijana ambao wamefanikiwa baada ya kupata mafunzo yale kwani wamejua kuchangamkia fursa. Wapo vijana wamepata Tenda kwenye Serikali kupitia ile sheeia ya PPRA, yote haya yalipatikana baada ya mafunzo tuliyoyafanya,kwahiyo ni fursa nzuri ambayo vijana wakiitumia vizuri wanaweza kufaidika".


Aidha Mhe Senyamule amesema kuwa lengo kuu la kongamano hili ni kuendelea kuona kundi hili kubwa la vijana linaendelea kuwekewa mikakati maalum ma kuelezwa namna Serikali inavyotenga fedha nyingi na kutengeneza fursa ambazo baadhi ya vijana bado hawazijui.


"Lengo kubwa kabisa la kongamano hili ni kuendelea kuona kundi kubwa la vijana likiwekewa mkakati maalum, pia kuwafanya vijana hawa ambao tayari wana ujuzi flani au elimu toka vyuo walivyosoma na kujiuliza cha kufanya waje kijifunza na kuona namna Serikali ilivyotenga fedha nyingi na kutengeneza fursa ambazo labda baadhi ya vijana bado hawazijui".



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Strategius Advisory Bi Lilian Mkumbo amesema kuwa kwa upande wao wamejitathmini na kuona kwamba muitikio  ni mzurina wameekuwa daraja la kuwasaidia watu kwa kuwakutanisha na wadau wa sekta ya Ajira na sekta ya Wajasiliamali.


"Kwahiyo tukijitathmini tunaona kwamba muitikio ni mzuri na tumekuwa daraja la kuwasaidia watu ,hatuwatafutii kazi ila tunawakutanisha wadau kwenye sekta ya ajira na sekta ya wajasiriamali maana pale wanafunguka na kupata kuona fursa mbalimbali,  hivyo tumejitathmini vya kutosha na tumeona ni namna gani hi hichi kitu kinahitajika kwa ukubwa".


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI