Header Ads Widget

WATUMISHI WA NCAA WANAOSHIRIKI SHIMMUTA JIJINI TANGA WATAKIWA KUZINGATIA NIDHAMU KWA KILA MCHEZO.



Na;Jusline Marco;Tanga


Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Dkt. Elirehema Doriye amesema kwa watumishi wa NCAA kushiriki michezo ni kwaajili ya kuimarisha afya zao, kujikingana magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanua  mtandao wa ushirikiano na taasisi nyingine.


Dkt.Doriye ameyasrma hayo wakati alipotembelea timu za NCAA zinazoshiriki mashindano ya SHIMMUTA Jijini Tanga na kusisitiza wachezaji hao kuzingatia nidhamu katika michezo yote wanayoshiriki.



Akizungumza na wachezaji wa NCAA wanaoshiriki michezo mbalimbali katika mashindano hayo, Dkt Doriye amebainisha michezo hiyo pia itasaidia NCAA kutangaza utalii wa ndani kupitia vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro kupitia washiriki wa michezo hiyo.


"Nawapongeza kwa jinsi mnavyoendelea kujitoa katika michezo mnayoshiriki,  nimemabiwa baadhi ya timu katika michezo kama Kamba (wanawake na wanaume) na mpira wa miguu, endeleeni kujitoa katika michezo hii lakini mhakikishe mnazingatia nidhamu kwa kila mchezo" amesisitiza Dkt. Doriye.


Michezo ya Shirikisho ya mashirika ya Umma na ya Sekta binafsi (SHIMMUTA) iliyofunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko ilianza tarehe 11 Novemba na itahitimishwa tarehe 22 Novemba, 2024  jijini Tanga.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI