Na Matukio damia Media App,Mbeya
DEREVA bodaboda mkazi wa IwambiJijini Mbeya ,Juma Afyusisye (38) anashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani hapa akidaiwa kumjeruhi kwa kummwagia petroli sehemu mbali mbali za mwili wake mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya msingi Iwambi kwa madai ya kutumia pesa aliyomtuma dukani kwa matumizi yake binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari November 8,2024 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema kuwa baada ya muathirika kurudi akiwa hana fedha ndipo mtuhumiwa alijichukulia sheria mkononi kwa kummwagia Petroli kwenye shati alilovaa na kisha kuwasha kiberiti na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.
"Mtoto huyu amelazwa hospitali Teule ya Ifisi katika Mji mdogo wa Mbalizi akiendelea kupatiwa matibabu "amesema Kuzaga .
Aidha Kamanda kuzaga amesema kuwa jeshi la polisi linatoa rai kwa wazazi na walezi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake watafute njia sahihi ya kuwaadhibu watoto pindi wanapokosea.
Kuzaga amesisitiza kuwa jeshi hilo halitavumilia wala kufumbia macho vitendo vya ukatili na unyanyasaji katika jamii, kieleza kuwa litaendelea kuchukua hatua kali kwa watuhumiwa kwa mujibu wa sheria.
0 Comments