Mbeya
WAKATI mchakato wa uchaguzi wa serikali ukiwa umewadia madiwani na wakuu wa wilaya Jijini Mbeya wameonywa kujiepusha na tabia ya kuingilia majukumu ya wasimamizi wa uchaguzi.
Hayo yamesemwa na Katibu tawala Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya ,Mohamed Fakii wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo uliopo katika kata ya Iwindi katika Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya mbeya.
“Tusiende kuingilia majukumu ya wasimamizi wa uchaguzi tuwaachie wasimamizi wafanye kazi zao zipo wilaya wameonekana wakuu wa wilaya na madiwani wanaenda kushughulika na masuala ya uchaguzi niseme hivi msimamizi anakuwa mmoja tu na maafisa wake na timu za uchaguzi ,sisi kazi yetu kwenda kutoa elimu na kuhimiza namna gani uchaguzi unaenda kufanyika “amesema .
Aidha Fakii amesema kuwa kazi ya uchaguzi sio kazi ya madiwani wala wakuu wa wilaya katika kusemea kazi ya uchaguzi wanaopaswa kusemea ni maafisa uchaguzi na msimamizi uchaguzi wanaofanya kinyume wanafanya makosa wakienda kusemea wanafanya makosa na kisheria haitakiwi kwani wanaweza kufanyiwa mapingamizi na kukatiwa rufaa na wao wanachotakiwa kufanya ni kuhamisisha watu wao kujiandaa namna ya kwenda kupiga kura.
Akielezea kuhusu vituo vya kupiga kura Fakii amesema kuwa maeneo ambayo yapo pembezoni viwekwe vituo vingi vya kupigia kura ili kurahisisha watu kuweza kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na TAMISEMI imeongeza vituo vya upigaji kura kwenye maeneo yenye shida ambayo yapo pembezoni na vituo havionekani wakati wa kujiandikisha kuna vituo vilikuwa havionekani ilikuwa changamoto hivyo hivi sasa vituo vitawekwa sehemu inayoonekana katika kurahisisha watu ili wapige kura .
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,Ezekia Shitindi amesema kuwa kazi ya madiwani ilikuwa kuhamisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari ambao ni wa vyama tofauti na itikadi tofauti .
“Hapa tuna halmshauri mbili ila hili lilosemwa na Katibu tawala hapa kwetu kwenye halmashauri yetu,kazi yetu sisi iliyobaki ni kuhamasisha wananchi wajitokeze November 27, mwaka huu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kuchagua viongozi “amesema Makamu Mwenyekiti huyo.
Maiko Ngailo ni Diwani wa Kata ya Bonde la songwe wilaya ya Mbeya amesema kuwa madiwani na wakuu wa wilaya wanaoingilia ni makosa kwasababu wanatakiwa kuwaacha watu wafanye kazi zao kuna mipaka na madiwani wanaoonekana kuingilia waache kwani kila kazi ina mipaka yake na madiwani wafanye kwa sehemu yao
0 Comments