Header Ads Widget

WAGOMBEA 9 WA CCM ARUSHA JIJI WAENGULIWA KUSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.

 

Jumla ya wagombea 9 wa Chama Cha Mapinduzi kwenye Halmashauri ya Jiji la Arusha Mkoani Arusha wameenguliwa kwenye mchakato wa Uchaguzi wa serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 kutokana na kutokidhi matakwa ya kikanuni na sheria za uchaguzi huo.

Kulingana na Msimamizi wa Uchaguzi, Wagombea hao wamekosa sifa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mitaa wanayogombea kutokuwepo kwenye orodha ya mitaa inayotambulika na Mamlaka ya serikali za mitaa pamoja na kutoainisha Jinsia zao kwenye fomu walizozijaza.

Miongoni mwa walioenguliwa ni pamoja na Frank Samwel Laizer aliyekuwa anagombea uenyekiti wa Mtaa wa Mbeshere, David Molel aliyekuwa anawania uenyekiti Mtaa wa Olkungu na Mohamed Amir aliyekuwa anawania Uenyekiti wa Mtaa wa Makaburi ya Baniani pamoja na Juma Waziri aliyekuwa mgombea Uenyekiti serikali ya mtaa wa Mkwangwaru B.

Aidha pia wamo wagombea wa Ujumbe wa serikali za mitaa akiwemo Hayrat Manyanga na Gilbert Massawe ambao pia wameshindwa kuendelea na uchaguzi huo wa baadae mwezi huu kutokana na dosari mbalimbali katika ujazaji wa fomu za kuwania nafasi hizo.

Chanzo:Arusha Zone

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI