Jimbo la Musoma Vijijini:
Jumla: Kata 21 Vijiji 68 Vitongoji 374
Matokeo:
(i) Vijiji 66: CCM
Vijiji 2: CHADEMA
Ushindi wa CCM: 97.06%
(ii) Vitongoji 357: CCM
Vitongoji 17: CHADEMA
Ushindi wa CCM: 95.45%
*Maendeleo ya wote:*
Matokeo ni hayo. Tusisahau kwamba sisi Musoma Vijijini huwa hatuna ubaguzi wa kisiasa na hatuna ubaguzi wa aina yo yote ile!
*Utekelezaji wa miradi ya maendeleo:*
Muhimu kwetu ni maendeleo shirikishi kwa manufaa ya jamii yote ndani ya vitongoji, vijiji na kata zetu zote.
Kuanzia wiki ijayo tunaendelea na utekelezaji wa miradi yetu iliyobuniwa na kuanza kutekelezwa kwa kutumia nguvu za wanavijiji. Baadhi ya miradi hiyo imeanza kupata michango ya fedha kutoka Serikalini
Miradi ni mingi, baadhi yake ni hii ifuatayo:
(i) ujenzi wa maabara 3 za masomo ya sayansi kwa kila sekondari ya Kata
(ii) ujenzi wa sekondari mpya kumi (10)
(iii) ujenzi wa shule shikizi nane (8) mpya
(iv) ujenzi wa zahanati mpya kumi na saba (17)
0 Comments