Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zikizinduliwa Rasmi Hapo Jana Nchini Kote Mjumbe Wa Kamati Kuu Ccm Taifa Halima Mamuya na Mlezi wa CCM Mkoa wa Njombe Amesema Salamu Za Mwenyekiti Wa Chama hicho Taifa Na Katibu Mkuu Ni Kuwa Hakuna Upinzani Tanzania Bali Wapo Waonyesha Changamoto Ambazo Zitakwenda Kufanyiwa Kazi Na Ccm Chini Ya Serikali Yake.
Akizindua Kampeni Hizo Kwa Mkoa wa Njombe Katika Uwanja wa Jeshi la Magereza Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe Mamuya amewaomba wananchi kuwachagua Viongozi wa Chama Hicho kwani wameshafanya makubwa na wanaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ambayo kila mmoja anaiona
Baadhi Ya Wagombea Wa Nafasi Ya Uenyekiti Wanawake Na Wanaume Akiwemo Francis Msanga Anayetetea kiti hicho Katika Mtaa wa Kambarage Wamesema Wanao Uwezo Wa Kufanya Kazi Kwa Ushirikiano Na Wananchi Wenyewe Pamoja Na Chama Na Hivyo Wanaomba Wawachague Wakawatumikie.
Naye Katibu Wa Siasa Na Uenezi Ccm Mkoa Wa Njombe Josaya Luoga Amesema Vijiji,Mitaa Na Vitongoji Vingi Vyama Rafiki Vimeshindwa Kusimamisha Wagombea Lakini Wao Wamefanikiwa Katika Maeneo Yote.
Katibu Wa Chama Hicho Mkoa Julius Peter Na Mwenyekiti Wake Deo Sanga Wamesema Wanatarajia Ushindi Mkubwa Katika Maeneo Yote Kwa Kuwa Ccm Imesimamia Vizuri Utekelezaji Wa Ilani Ya Uchaguzi Na Serikali Imeleta Fedha Nyingi Za Miradi Ya Maendeleo.
Kwa upande wao Wananchi Mkoani Njombe akiwemo Joshua Nyigu wamekiomba Chama Cha Mapinduzi kwenda Kushughulikia Changamoto zinazowasibu vijana wengi nchini hususani Ajira pindi watakapochaguliwa.
Novemba 27 Mwaka huu Inakwenda Kupigwa kura ya kuwachagua viongozi mbalimbali wakiwemo Wenyeviti wa vijiji,Mitaa,Vitongoji na Wajumbe wa Serikali za Mitaa.
0 Comments