Na,Jusline Marco;Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Amir Mkalipa ameitaka idara ya manunuzi kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya mifumo ya fedha ili kuweza kuondoa changamoto ndogondogo zinazowakabili watumiaji wa mifumo hiyo.
Mkalipa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika kikao cha pili cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Meru ambapo amesema ili changamoto hiyo iondoke lazima watu wa manunuzi wawajibike ipasavyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Jeremia Kishili katika kikao hicho amekiri kuwepo kwa fedha ambazo hazijatumika katika baadhi ya mihula ambapo amesema kila baada ya miezi mitatu watakuwa wanapata taarifa ya matumizi ya fedha za mapato ya ndani ili kuhakikisha fedha hizo zinatolewa kwa muda unaotakiwa.
Naye Katibu Tawala Msaidizi Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi Mkoa wa Arusha CPA Ramadhani Madeleka amesema suala la ukusanyaji wa mapato katika halmashauri ni agenda ya kudumu ambapo amesema kama mkoa agenda yao ni kila halmashauri kufikisha zaidi ya asilimia 50 ya ukusanyaji wa mapato.
Mbali na hayo CPA Madeleka amewataka wataalam, wakuu wa idara husika pamoja na wakuu wa taasisi kushiriki katika vikao vya baraza la madiwani na kutoa majawabu sahihiya maswali yatakayoulizwa na madiwani ili kurahisisha vikao kwenda kwa urahisi.
0 Comments