Header Ads Widget

VIJANA WATAKA MKAKATI WA KIMATAIFA KULIOKOA BARA LA AFRIKA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Vijana wanaharakati  wa mazingira  wameshauri kuwepo kwa mkakati wa kimataifa wa kuliokoa bara la Afrika kutokana na athari za uharibifu wa mazingira yanayochangiwa na mataifa yaliyoendelea.


Wametoa ushauri huo katika mkutano wa Haki ya Mazingira uliowakutanisha vijana kutoka mataifa zaidi ya 100 Duniani, mkoani Arusha uliolenga kujadili mbinu endelevu za kupunguza athari za uharibifu wa wazingira.


Faustine Lusanzu alisema kuwa kuelekea mkutano mkuu wa mazingira wa Umoja wa Mataifa unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao wanaamini viongozi watakaokutana watafanyia kazi ushauri huo hivyo wanatuma sauti zao na huenda mabadiliko ya tabia  yakabaki kuwa historia.


Ziada Kassim mwanaharakati wa mazingira alisema kuwa athari za mabadiko ya nchi zinaendana katika maeno mbalimbali hasa Afrika hivyo wanapokutana pamoja wanatoka na majawabu yanayoendana jambo linalosaidia kuleta mabadiliko


"Tunajua kuwa vijana ni wengi katika nchi zetu kwahiyo tunaongeza nguvu kubwa katika kupambana na athari hizi na kupitia mkutano huu tumepata mawazo na majawabu mengi ambayo yataenda kusaidia katika mkutano wa umoja wa mataifa kudai haki zetu za kimazingira tulizoadiwa lakini pia kurudi katika nchi zetu kwenda kuwasilisha tuliyojifunza," Alisema Ziada.

"Athari za mabadiliko ya tabia  hazinihusu tu mimi niliyehudhuria mkutano bali inatuhusu wote kwa mfano kwa nchi yangu ya Tanzani Rais wetu Mh Samia Suluhu amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunaenda sambamba na mikakati ya tabia ya nchi hivyo tuungane pamoja, tuwe kitu kimoja kwani athari hizi zinamuhusu kila mmoja, majuzi  tumekumbwa na mafuriko na kuna ukame na kuna hatihati baada ya miaka kadhaa tunaweza kuwa na uhaba wa chakula,"Alisisitiza.


Happiness Njile alisema vijana ni kundi linalosambaa kila sekta hivyo athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ni jambo linalowakabili na linahitaji ufumbuzi hivyo wapo katika mkutano huo kuona kila nchi ina athirika vipi na nini kifanyike kuondoka na madhara hayo.


"Binafsi kupitia mkutano huu nimejifunza juu ya uelimishaji, ushirikishwaji wananchi katika utunzaji wa mazingira ili tuweze kujiweka sawa na kuondokana na athari za mabadiliki ya tabia ya nchi,"Alisema.


Kwa upande wake Agus Naggio Mratibu wa mkutano wa haki ya mazingira  alisema kuwa  wanachokifanya ni kuunda nafasi kwa viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kukusanyika na kuchukua hatua za pamoja  katika kukabiliana na athari hizo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanatoa fursa nyingi kwa kadri inavyowezekana kwa vijana ili waweze kurudi katika jumuiya zao na kuendelea kuhamasisha hatua za kuchua  kupambana na tabia ya nchi.


"Tumeona shida ya hali ya hewa ikiwaathiri vijana wengi katika kambi hii na katika jumuiya zao na tunatka kuunda nafasi ambazo wataweza kushuriki hadithi hizo za kibjnafsi na kutafuta ufumbuzi na tayari tunajadii mipango ya siku zijazo," Alieleza Naggio.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI