NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah amesema kwamba, ujio wa Mufti Ismail Menk kutoka nchini Zimbabwe na jopo la Masheikh zaidi ya 18 kutoka mataifa mbalimbali Duniani limetoa fursa kwa Zanzibar kujitangaza zaidi kupitia utalii wa maadili (Halali Toursim).
Makamu wa Pili amesema hayo wakati akifunga hafla ya Jukwaa la kwanza Aftika la Uwekezaji wa Utalii wa Maadili (Halali Tourism) uliowakutanisha Mashaikh, Wahadhiri na wana vuoni kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni kote.
Amesema, kwa kipindi cha Siku Tatu ambacho Mufti Menk na jipo wapo Visiwani Zanzibar zaidi ya Watu Milioni 10 wamekuwa wakifuatilia hotuba zake kupitia makongamano aliyoshiriki na kuifanya Zanzibar kufungua fursa zaidi katika kuwekeza katika utalii.
Aidha, amefahamisha kuwa Serikali kupitia Kamisheni ya Utalii inaendelea kufanya mapitio ya mwisho ya Sera ya Utalii ya Zanzibar ya Mwaka 2017 kwa lengo la kuifanyia maboresho ikiwemo eneo la Utalii wa maadili kwa kuweka mikakati mbili mbali itakayosaidia kukuza utalii wa kiislam hapa Zanzibar.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemuahidi Mufti Menki na ujumbe wake kuwa Serikali na waislamu kwa ujumla watayafanyia kazi yale yote waliyojifunza kutoka kwako na kuwataka kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Zanzibar kiutalii hasa katika Utalii wa maadili na kuwahamasisha wataalamu mbali mbali wa Kiislamu kuja Zanzibar kufanya Tafiti za historia ya kiislam zitakazosaidia kuitangaza dini na Zanzibar kwa ujumla.
Aidha Makamu wa Pili amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu mbali mbali ikiwemo ya barabara, Viwanja vya ndege na Bandari ambavyo vinachochea ukuwaji wa sekta ya Utalii nchini.
Nae Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadhan Soraga ameishukuru Kampuni ya Light upon Light kwa kuamua kufanya Jukwaa la Utalii wa maadili Visiwani Zanzibar ambalo litasaidia katika kuitangaza Zanzibar kiutalii na kutanua wigo kwa wageni wengi zaidi kuitembelea Zanzibar.
Soraga amesema Jukwaa la Utalii wa maadili ni muhimu katika maendelea ya Zanzibar na kila kilichojadiliwa katika Jukwaa hilo kinalenga katika kuiendeleza Zanzibar kiutalii na kuifanya kuwa Kituo kikubwa cha Utalii Barani Afrika, hivyo atahakikisha kuwa Wizara inachukua juhudi za maksudi kuviboresha vivutio vya utalii na kuanzisha vipya ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea.
Kwa wake Mufti Ismail Menk ameishuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wananchi kwa ujumla kwa mapokezi ya heshima, upendo na ukarimu walionaompatia yeye na ujumbe wake jambo linalompa faraja ya kuendelea kuitembelea tena Zanzibar na kuahidi kutangaza mazuri yote waliyojifunza Zanzibar .
Amesema kuwa, kila binaadamu ana wajibu wa kuzitumia neema alizojaaliwa na Allah katika kuisimamia Dini ya kiislam na kuwa tayari kutoa neema hizo kwa ajili ya kuwasaidia wasio na uwezo na wenye mazingira magumu kwa kutambua hilo ndio lengo la kuletwa kwake Duniani kuja kumtumikia Allah (S.W).
Amesema, miongoni mwa Ibada anazotakiwa kufanya muislamu ni kufanya kazi ya halali kwa kufuata misingi ya Dini ya kiislamu jambo litakalosaidia waislamu kuishi kwa upendo na kusaidiana pamoja na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Mapema Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kiislamu wa Benk ya KCB Amour Muro amesema kuwa Wataendelea kuwekeza na kuunga mkono jitihada za Serikal katika kuandaa Makongamano yenye kujuza utali wa halali.
0 Comments