Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP.
WAZIRI MKUU amewataka Watumishi wa Halmashauri Nchini kuendelea kuweka mikakati ya kushirikisha Sekta binafsi katika mipango ya Kimaendeleo.
Mhe.Kassim Majaliwa amesema hayo Oktoba 06,2024 alipozungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaaya Kinondoni ,Jijini Dar es salaam kwenye Ukumbi wa chuo cha Maendeleo ya Wananchi.
Mhe.Waziri Mkuu yupo Jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kuwataka Watumishi wa Halmashauri ya Manispaaya Kinondoni kuweka chachu ya Maendeleo kwa Wananchi kupitia Sekta binafsi.
"Sera yetu ndani ya Serikali inahamasisha Sekta binafsi kuwekeza na kutoa huduma,katika idara yao ni lazima ujiulize imechangia kiasi gani katika kutoa huduma." Alisema Waziri Mkuu.
Aidha Mhe. Majaliwa amewataka madiwani kwenye Halmashauri zote Nchini kushiriki katika kufanya makadirio ya makusanyo kwenye Halmashauri zao kwa kushirikiana na Watendaji wa Halmashauri,Kata na Vijiji .
"Baraza la madiwani kafanyeni Survey ili mvitambue vyanzo vyote na mjue na kujiridhisha vinachangia kiasi gani,nendeni mkajifunze Temeke namna wanavyofanya , walivyo pandisha makusanyo kutoka milioni 8 kwa wiki mpaka milioni 120" Alisema Mhe.Majaliwa.
............ Mwisho...........
0 Comments