Header Ads Widget

RPC SONGWE AELEZA UTAYARI WA ASKARI WAKE KUZUIA UHALIFU




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga, amesema Jeshi la Polisi limesema linaendelea kudumisha mahusiano na wananchi kwa kuzingatia dhana ya Polisi Jamii ili kuhakikisha wanafichua wahalifu katika mkoa wa Songwe na kupunguza vitendo vya uhalifu na wahalifu.



Kamanda Senga amebainisha hayo wakati akifanya ukaguzi wa mafunzo ya utayari tarehe kwa Askari polisi jumatano hii (Oktoba 02, 2024) iliyofanyika katika uwanja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.



Kamanda Senga amesema Songwe inakwenda kupunguza matukio ya uhalifu na wahalifu ikiwa ni pamoja na ukatili wa kijinsia kutokana na mipango endelevu ya kuwalinda raia na mali zao kwa kuendelea kufanya mazoezi ya utayari ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mambo mbalimbali ya usalama.



Aidha, Kamanda amewataka Askari wa Mkoa wa Songwe kuendelea kufanya kazi kwa nidhamu, haki, weledi na uadilifu ili kuendelea kuaminiwa na jamii na kulinda taswira nzuri ya Jeshi la Polisi.



Mafunzo hayo yamedumu kwa kipindi cha mwezi mmoja na yanalenga kuboresha afya ya mwili na akili ili kuhakikisha askari hao wanatekeleza majukumu yao kwa weledi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI