Header Ads Widget

DC NJOMBE: VIJANA WAACHE KUKIMBIA NA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA MAPATO YA NDANI

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati serikali ikitangaza kurejea kwa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani,Halmashauri ya mji wa Njombe Imetenga kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya vijana,wanawake na wenye ulemavu.


Wakati akifungua mafunzo kwa maofisa maendeleo ya jamii Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Kasongwa amesema uongo na uaminifu duni kwa vijana wengi katika mikopo hiyo unawarudisha nyuma na kukwamisha jitihada za kujiletea maendeleo hivyo wanapaswa kuwa waaminifu.



Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Kuruthum Sadick amesema maofisa maendeleo ya Jamii watapatiwa mafunzo ili waende kuhamasisha vikundi na kuvisajili.


Enembora Lema ni mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Halmashauri ya mji wa Njombe ambaye anasema kuna utaratibu mpya ambao umetolewa katika utoaji mikopo hiyo hivyo watakwenda kutoa elimu mtaa kwa mtaa na kijiji kwa kijiji.


Mwenyekiti wa Umoja wa vijana mkoa wa Njombe Samuel Mgaya amesema anatamani kuona vijana wanapata mkopo wenye tija katika maeneo yote ya mkoa na hivyo iwe fursa kwao kunufaika na mikopo hiyo huku Mwenyekiti wa Vijana wa CCM wilaya ya Njombe Erick Ngole kwa niaba ya vijana akiahidi kuwahamisha vijana kuwa waaminifu katika kurejesha fedha hizo.



Wananchi mkoani Njombe wanasema kurejeshwa kwa mikopo hiyo kutakwenda kuwasaidia kuongeza mitaji yao katika biashara na kuwakwamua kiuchumi.


Mikopo hiyo ilisitishwa mwaka 2023 Aprili kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo Udanganyifu wa uundaji vikundi,Kutorejeshwa kwa mikopo hasa kwa kundi la Vijana pamoja na Madiwani kutajwa kujikopesha fedha hizo badala ya kundi lengwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI