Header Ads Widget

MAONESHO MAKUBWA YA DHAHABU KUFANYIKA SONGWE

 


Na Thobias Mwanakatwe


Wachimbaji madini na wananchi kwa ujumla wa ndani na nje ya wilaya na mkoa wa Songwe wametakiwa kujitokeza kushiriki maonesho ya dhahabu yatakayofanyika wilayani humo kuanzia Oktoba 12 hadi 14 mwaka huu.


Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Solomon Itunda, akizungumza jana 01/10/2024 amesema maonesho hayo ya dhahabu yatafanyika katika kata ya Saza.


"Nitumie nafasi hii kuwaalika wananchi wote wa Wilaya ya Songwe, Mkoa wa Songwe na Watanzania kwa ujumla wajitokeze kushiriki maonesho haya muhimu kwa maslahi mapana ya taifa letu na sekta ya madini," amesema.



Amesema maonesho hayo ambayo yameandaliwa na Mc Edwin Luvanda Branding and Entateiment Company, yatafuatiwa na tamasha litakalofanyika Oktoba 14, 2024 litakalofanyika mjini Chunya kwenye ukumbi wa Omari Hotel.


Mkuu huyo wa Wilaya amesema wakati wa maonesho hayo, wachimbaji wadogo,wa kati na wakubwa watapata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa namna kufanya kazi za uchimbaji.


Ameongeza kuwa pia wakati wa maonesho hayo wachimbaji wataweza kuonyesha zana mbalimbali wanazozitumia katika shughuli za uchimbaji madini.


Itunda amesema kwenye tamasha yapo makundi mbalimbali ya wachimbaji ambayo yatapewa tuzo wakiwamo wachimbaji chipukizi na wachimbaji wanaolipa kodi kwa uaminifu serikalini.


Aidha, wakati wa maonesho hayo washiriki watapewa elimu na watu kutoka Wakala wa Usalama wa Afya Mahala pa Kazi (OSHA) na taasisi za fedha ambazo ni pamoja na Benki ya CRDB na NMB.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI