Header Ads Widget

MIKUTANO YA KAMPENI KUTUMIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa itatumia mikutano hadhara ya kampeni ya vyama vya siasa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuendesha kampeni na kutoa elimu ya kupambana na rushwa.

 

Afisa Elimu kwa umma TAKUKURU mkoa Kigoma, Ibrahim Sadiki alisema hayo katika semina ya siku moja kwa waandishi wa Habari wa mkoa Kigoma kuhusu kampeni ya kupinga vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa.

 

Sadiki alisema kuwa kutumika kwa njia kunatokana na mafanikio makubwa ambayo TAKUKURU imeyapata katika kuendesha kampeni zake za elimu kwa umma kwa kutumia mpango wa TAKUKURU Rafiki ambapo waliweza kutumia mikutano ya hadhara na kupitia vikundi mbalimbali ambapo elimu ya kupambana na rushwa ilifanikiwa kupenya kwa jamii.

 


Akizungumza katika semina hiyo Mwanasheria wa TAKUKURU mkoa Kigoma , Jackson Lyimo alisema kuwa Pamoja na mikutano kuleta mafanikio makubwa katika kupatikanaji wa taarifa za rushwa pia waandishi wa Habari wamekuwa na mchango mkubwa katika kuibua vitendo na viashiria mbalimbali vya rushwa mkoani Kigoma.

 

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari mkoa Kigoma (KGPC), Jacob Ruvilo alisema semina kama hizo zina manufaa makubwa na kuwapa uelewa mambo mbalimbali lakini kuwafanya TAKUKURU na waandishi wa Habari kufanya kazi Pamoja kama timu na kupeana mipaka ya kazi na majukumu yao.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI