Header Ads Widget

MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO YASHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI MITI KWENYE TAMASHA LA LAND ROVER JIJINI ARUSHA.

 

Na,Jusline Marco;Arusha

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kupitia maafisa waandamizi  wake imeshiriki Shughuli ya utunzaji mazingira kwa zoezi la upandaji miti katika eneo la uwanja wa  Magereza Kisongo jijini Arusha.

Afisa Mhifadhi Mwandamizi Idara ya Uhusiano wa Umma kutoka katika hifadhi hiyo Kasimu Nyaki akizungumza katika hitimisho la Tamasha la Land Rover lililoratibiwa na mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda yaliyofanyika kwa siku tatu yenye lengo la utangaza utalii.


Nyaki amesema ushiriki wa NCAA katika zoezi hilo ni sehemu ya kuendana na Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na kuhifadhi mazingira kama sehemu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira katika mkoa wa Arusha.


Katika hatua nyingine Nyaki ameeleza kuwa Mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro imeshiriki kwenye tamasha la Magari ya Land Rover yaliyoratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ikiwa ni uungaji mkono juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan za kutangaza Sekta ya Utalii Duniani.


Aliongeza kuwa NCAA kama  wadau wa utalii matumizi ya gari aina ya Land Rover ni moja ya magari yanayotumika katika eneo la hifadhi kwenye shughuli mbalimbali za kiutalii na utafiti ambapo kupitia wizara mama ya maliasili na utalii imetumia fursa ma tamasha hilo kukutana na wananchi mbalimbali kutoa elimu kuhusiana na masuala ya uhifadhi na shughuli zinazofanyika ndani ya hifadhi ya ngorongoro ikiwemo vivutio vya utalii vilivyopo.


"Sambamba na utoaji wa elimu hiyo pia tunaelezea shughuli za maendeleo ya jamii ambazo tunazifanya ndani ya hifadhi ya Ngorongoro na nje,lakini pia kuelezea fursa za uwekezaji katika maeneo mbalimbali ndani ya hifadhi ya Ngorongoro."Alisema Afisa huyo


"Kwa ujumla tamasha hili limetupa nafasi kubwa ya kuendelea kukutana na wadau wetu hususani watalii wa ndani na nje pamoja na wananchi wa mkoa wa Arusha ambao wamekuwa wakitembelea katika tamasha hilo kupata elimu mbalimbali kuhusiana na masuala ya Utalii na tamasha hili limekuwa na manufaa makubwa sana katika kuwafikia wananchi kupitia shughuli mbalimbali."Alisistiza Kasimu Nyaki Afisa Mhifadhi Mwandamizi Idara ya Uhusiano wa Umma NCAA.



Tamasha hilo la Land Rover 2024 ambalo lilianza Oktoba 12 limehitimishwa Oktoba 14 kwa zoezi la upandaji miti zaidia ya 500 katika eneo la Uwanja wa Magereza uliopo Kisongo jijini Arusha ambapo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa ameongoza washiriki wa Tamasha hilo katika upandaji wa miti ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kumbukizi ya miaka 25 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Awali Mkuu huyo wa Wilaya ameeleza kuwa siku tatu za Tamasha hilo  zimekuwa na matokeo chanya kwenye uchumi wa Mkoa wa Arusha kwa wajasiriamali wadogowadogo na wafanyabiashara mbalimbali kutokana na ugeni wa watu zaidi ya 3000 ambao wamekuwa wakitumia fedha zao kwenye manunuzi na matanuzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI