Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana (Mb) amewasili katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro tayari kwa tukio la kupandisha mwenge wa Uhuru katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro, Zoezi ambalo linafanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Waziri Chana, amepokelewa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii, Nkoba Mabula, Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Juma Kuji pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Chama na Serikali.
Mwenge wa Uhuru unapandishwa leo katika kilele cha Mlima Kilimanjaro Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mbio za mwenge huo na ikiwa ni mara ya pili tangu kupandishwa 1961.
#MwengeUmerudiNyumbani#2024
0 Comments