Na Shemsa Mussa
Kagera.
Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa [FAO] limekuja na mbinu na Teknolojia mpya ya umwagiliaji wa mbogamboga ili kudumisha Zaidi suala la lishe na kutokomeza udumavu na utapiamlo kwa wananchi wa Mkoa huo.
Akizungumza katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya chakula duniani Bi,Theresia Massoy Mwakilishi Mkazi wa shirika hilo ambaye pia ni Mshauri wa masuala ya kilimo ndani ya shirika kutoka katika kituo cha Kigoma,amesema wao kama shirika wamekuja na teknolojio hiyo ambayo itamsaidia mkulima pamoja na mama mjamzito kuhakikisha mtoto aliyomo tumboni anazaliwa bila utapiamlo.
‘’Hapa Tumeangalia teknolojia ambayo itamsaidia mkulima na mama ,lakini ni mama yupi mama ambaye yupo katika jiko lake anataka kuhakikisha katika hali ya ujauzito anazalisha chakula ambacho kinalenga kumpa yeye lishe bora na mtoto atakayezaliwa awe na afya bora basi atakuwa na bustani yake ambayo sisi tumemtengenezea mazingira mazuri hata choka kumwagilia,amesema Bi Theresia’’
Pia amasema kwa hatua hiyo watahakikisha kila kaya inapata taknolojia rahisi itakayorahisisha kuzalisha kwa usahihi na kwa ufanisi bora Zaidi wa mbogamboga ambazo vitamin zinapatikana katika mimea hiyo Iikiwemo Vitamin C inayosaidia katika mmeng’enyo wa chakula,huku akisema katika mlo huo si kwa ajili ya mama mjamzito pekee bali hata watoto walioacha kunyoya na walio chini ya miaka mitano.
Katika kumrahisishia kazi mwananchi hasa Mama shirika hilo la chakula na kilimo la umoja wa mataifa FAO limeweza kuwapatia vifaa mbalimbali ikiwemo mifumo 40 ya umwagiliaji, pia ili mkulima kuepuka changamoto za umwagiliaji wa baadhi ya mimea wametoa vifaa 40 vya umwagiliaji.
‘’Pamoja na ugawaji wa vifaa hapa katika zahanati ya kibeta kumeshuhudia usomaji wa taarifa unaoonesha hali halisi ya upatikanaji wa chakula na matumizi ya hii teknolojia rahisi na tumeona bustani ya mbogamboga katika kituo hiki basi washiriki wote hapa wameweza kuona vifaa hivi vilivyogawiwa vinafanyaje kazi kwa hiyo wamejua namna ya kuunganisha mitambo hii modogo na kuona matayarisho ya vyakula mbalimbali,ameongeza Bi Theresia’’
Nao baadhi ya wananchi waliohudhulia katika maadhimisho hayo akiwemo Mariam Marichory wameliomba shirika hilo kuzidi kutoa elimu na vifaa vitakavyowasaidia kupata afya bora na miili yenye nguvu na kuepuka utapiamlo na udumavu uliokithiri.
0 Comments