NA MWANDISHI WETU
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama dcha Act Wazalendo Ismail Jussa Ladu maesema Rais Mstafu Dkt Salmini Amour Juma ataendelea kukumbukwa kwa uwamuzi wake wa kutaka Zanzibar kuwa mwananchama wa Shirikisho la Kislaam (OIC) na Zanzibar kuwa Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojitegemea kama nchi.
Juss ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Jimbo la Kojani Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Aliasema kitendo cha Zanzibar kuzuiwa kujiunga na oic kilirejesha nyuma maendeleo ya Zanzibar kwa vile nchi nyingi zilizojiunga na Shirikisho lile zilinufaika na miradsi mbalimbali ikiwemo Elimu na ustawi wa jamii.
Alisema kwamba, Zanzibar bila ya kuwa na Mamlaka kamili haiwezi kusonga mbele ndio maana Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad alisimamam imara na wenzake kutetea maslah ya Zanzibar ndani ya mfumo wa Muungano na kufikia kufukuzwa ndani ya chama cha Mapinduzi CCM.
“Maalim Seif na wenzake walifukuzwa kuonesha msimamo wa kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya Mfumo wa Muungano lakini badala yake wakashtakiwa katika kikao cha Halmashauri Kuu kuwa wanasaliti msingi ya Ujamaa na kujitegema” alisema Jussa.
Alisema Msimamo wa Maalim Seif wa Zanzibar kuanzishwa soko huru la biashara ulisaidia Zanzibar kufunguka kiuchumi na Wananchi kupata unafuu wa kupata bidhaa mbalimbali ikiwemo chakula.
Aidha alisema kwamba Maalim Seif ndie alieeibua Zanzibar kuwa na nembo yake ya Serikali,Bendera ya Taifa ya Zanzibar kama kielelezo cha nchi badala ya kutumia nembo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Adam na hawa na bendera ya Taifa ya Tanzania.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Act Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman amesema ripoti ya Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) imekwama kutekelezwa tangu kukabidhiwa na tume ya fedha ya pamoja mwaka 2006 kutokana na kukosekana nia ya njema ya kumaliza kero za Muungano.
Alisema mpango wa uanzishwa kwa tume ya pamoja ya fedha kupitia vyanzo vya mapato ya muungano na kuweka mfumo wa mgao uliibuliwa na aliekuwa Rais wa Zanzibar Dkt Salmin Amour mwaka 1996 lengo Zanzibar kupata haki zake ndani ya Muungano.
Alisema lengo kubwa ilikuwa ni kujua mapato ya Muungano yanakusanywa na kufahamu matumizi ya Muungano na kinachobakia kuweka mfumo wa mgao ambao Zanzibar inastahiki kupata.
“Mwaka 1996 kulipitishwa dsheria Tume ya pamoja ya Fedha na baada ya karume kuingia madarakani na tume hiyo ikaanzishwa mwaka 2003 ambapo mwaka 2006 Tume iliwasilisha ripoti ikionesha mabilioni ya Fedha ambayo Zanzibar inastahili kuyapata kutokana na Muungano,”
Othman ambae alisema yeye alikuwa mionmgoni mwa wajumbe wa Tume hiyo ambae alifanya kazi kwa zaidi ya miaka 10 lakini tangu tume hiyo kumaliza muda wake 2018 haijaundwa tena wala utekelezi wa ripoti yake.
AIdha alisema kwamba Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Aman Karume ndie wa kwanza kupambania maslahi ya Zanzibar ikiwemo kukataa fedha ya Zanzibar kuhifadhiwa kwenye Muungano na kuamua kuanzisha benki ya watu wa Zanzibar.
Nae Naibu katibu Habari na Mawasiliano ya Umma Salum Biman ameshangazwa na kitendo cha Wajumbe wa baraza la Wawakilishi kushindwa kujitokezav kuhoji Serikali tuhuma 27 za ufisadi katika miradi ya Serikali na kero 41 za Muungano mambo ambayo yameelezwa na Act Wazalendo tangu kuanza kwa mikutano.
Chama cha Act Wazalendo kimehitisha awamu ya pili ya mikutano ya hadhara kisiwani Pemba ambayo imeibua mijada mikubwa kwa wafuasi wa chama hicho katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na muelekeo wa hali ya kisiasa Zanzibar.
0 Comments