NA MWANDIDHI WETU
MWENYEKITI wa Chama cha Act Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman amesema ripoti ya Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) imekwama kutekelezwa tangu kukabidhiwa na tume ya fedha ya pamoja mwaka 2006 kutokana na kukosekana nia ya njema ya kumaliza kero za Muungano.
Othman Masoud Othman aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Jimbo la Kojani Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema mpango wa uanzishwa kwa tume ya pamoja ya fedha kupitia vyanzo vya mapato ya muungano na kuweka mfumo wa mgao uliibuliwa na aliekuwa Rais wa Zanzibar Dkt Salmin Amour mwaka 1996 lengo Zanzibar kupata haki zake ndani ya Muungano.
Alisema lengo kubwa ilikuwa ni kujua mapato ya Muungano yanakusanywa na kufahamu matumizi ya Muungano na kinachobakia kuweka mfumo wa mgao ambao Zanzibar inastahiki kupata.
“Mwaka 1996 kulipitishwa dsheria Tume ya pamoja ya Fedha na baada ya karume kuingia madarakani na tume hiyo ikaanzishwa mwaka 2003 ambapo mwaka 2006 Tume iliwasilisha ripoti ikionesha mabilioni ya Fedha ambayo Zanzibar inastahili kuyapata kutokana na Muungano,”
Othman ambae alisema yeye alikuwa mionmgoni mwa wajumbe wa Tume hiyo ambae alifanya kazi kwa zaidi ya miaka 10 lakini tangu tume hiyo kumaliza muda wake 2018 haijaundwa tena wala utekelezi wa ripoti yake.
AIdha alisema kwamba Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Aman Karume ndie wa kwanza kupambania maslahi ya Zanzibar ikiwemo kukataa fedha ya Zanzibar kuhifadhiwa kwenye Muungano na kuamua kuanzisha benki ya watu wa Zanzibar.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Chama dcha Act Wazalendo Ismail Jussa Ladu alisema Rais Mstafu Dkt Salmini Amour Juma ataendelea kukumbukwa kwa uwamuzi wake wa kutaka Zanzibar kuwa mwananchama wa Shirikisho la Kislaam (OIC) na Zanzibar kuwa Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojitegemea kama nchi.
Alisema hata hivyo mpango huo ulikwama baada ya mwalimu nyerere kupinga jambo hilo wakati lilikuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi kwa Zanzibar na kusababisha Zanzibar kukwama kujiunga na shirikisho hilo.
Nae Naibu katibu Habari na Mawasiliano ya Umma Salum Biman ameshangazwa na kitendo cha Wajumbe wa baraza la Wawakilishi kushindwa kujitokezav kuhoji Serikali tuhuma 27 za ufisadi katika miradi ya Serikali na kero 41 za Muungano mambo ambayo yameelezwa na Act Wazalendo tangu kuanza kwa mikutano.
Chama cha Act Wazalendo kinaendelea na mikutano yake ya hadhara huku wakitumia nafasi mbalimbali kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia kwa kuruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara baada ya kuzuiwa kwa miaka saba chini ya uongozi wa Marehemu Dkt John Pombe Magufuli.
0 Comments