Na Matukio Daima media
Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoani Arusha Festo Kiswaga ametoa muda wa Siku 90 kwa fundi anayejenga nyumba ya Walimu shule ya msingi Loorela kukamilisha ujenzi huo.
Pamoja na kumpa muda huo fundi pia amemtaka Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kufuatilia ujenzi huo na kuhakikisha inakamilika kwa ubora wa Viwango vya serikali .
Kiswaga alitoa agizo hilo Jana baada ya kufika Kijijini hapo kuhamasisha wananchi kushiriki ujenzi wa nyumba hiyo itakayovutia mazingira bora ya makazi ya Walimu ili kukuza ubora wa elimu wilayani hapo.
"Nimegundua Wananchi wa Kijiji cha Loorela wakulima na wafugaji hawana shida katika kuchangia miradi ya maendeleo katika eneo lao hasa katika hili la u jenzi wa nyumba ya walimu."
Hata hivyo apongeza utayari wa Walimu kwani baaada ya kuomba kujengewa nyumba tayari wamechukua hatua ya kuleta kokoto, mchanga bila hata kusubiria.
Kiswaga amepongeza jitihada Kuwa za serikali ya awamu ya sita chini Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa za kusogeza maendeleo kwa wananchi hata kutoa pesa nyingi Monduli ili tuhakikishe zinatumika kama zinavyokusudiwa kwa maendeleo ya wana Loorela Wilayani Monduli.
Alisema ujenzi wa nyumba hiyo ya walimu (two in one) utagharimu kiasi Cha Tsh.92.4 fedha zilizotolewa na Rais Dkt Samia.
Kuwa nyumbani hiyo itakuwa ni Ukombozi katika Shule ya Msingi Loorela ambacho ni miongoni mwa vijiji vinavyonufaika na mpango wa kaya maskini inayotarajiwa kuwa na vyumba vitatu (3) vya kulala.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo Bi.Crensia Pius Shine ambaye ni Mratibu wa TASAF Wilaya ya Monduli amesema
Kuwa Shule hiyo ya Loorela ina jumla ya wanafunzi 269 na walimu watatu watatu hivyo mradi huo wa thamani ya milioni 92.4 uliotolewa na TASAF awamu ya tatu na OPEC awamu ya nne ni matunda ombi ya wananchi hao lililoibuliwa Oktoba 12, 2022 katika mkutano mkuu maalum wa wananchi hao.
Wananchi hao walikubaliana kuchangia nguvu kazi pamoja na mawe, kokoto, Mchanga, Maji, pamoja na kulinda vifaa vyote vitakavyonunuliwa na kuhifadhiwa katika eneo lao."

Happiness Laizer Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ametoa Rai kwa wananchi kutunza vifaa vya ujenzi vizuri na hata ujenzi ukikamilika vitakavyobaki virudishwe ghalani kwa matumizi mengine baadae.
Alisema kuwa kupatikana kwa nyumba ya walimu kutaleta tija katika Shule yetu ya Loorela sambamba na kuimarisha utaratibu wa usalama wa Mali za Serikali zilizopo shuleni hapo kutokana na uwepo walimu katika maeneo ya Shule kila wakati.
Kwa upande wake Johnson Loleku Mwalimu Mkuu wa Shule ya Loorela amefurahishwa sana kupata mradi huu kwani jambo hili litapunguza adha ya walimu kutoka mbali kuja shuleni kuendelea na shughuli zao za ufundishaji.
Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoani Arusha Festo Kiswaga akishiriki ujenzi wa nyumba Moja itakayotumiwa na Walimu watatu shule ya msingi Loorela picha na Matukio Daima media
0 Comments