Makam mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM bara na Waziri Mkuu mstaafu John Malecela amewasihi wananchi kujitokeza kwenye uandikishaji daftari la makazi iliwaweze kutumia haki yao ya msingi wa demokrasia katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumza na radio kicheko live Mheshimiwa Malecela amesema Tanzania ni Nchi ya demokrasia na imekuwa ikifanya vyema katika kusimamia demokrasia hiyo kwakuzingatia taratibu na katiba yake kila inafika kipindi cha uchaguzi na wananchi wamekuwa wakichagua viongozi wanaoona watawaletea maendeleo.
Amewataka wananchi kote Nchini kujitokeza kwenye uandikishaji daftari la makazi iliwaweze kukidhi vigezo vya kuwa wapiga kura halali huku akiwasihi pia watanzania kujitokeza siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 27 November iliwaweze kuchagua viongozi wanaowataka.
Aidha mheshimiwa Malecela ametoa wito kwa kundi la vijana kujitokeza kwa wingi kwenye uandikishaji huo huku pia akiwahimiza vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kuachana na dhana ya kutengeneza makundi na kuilaumu serikali.
"Demokrasia ni utawala unaotokana na kura na ni utawala wa kupokezana madaraka kwa kuchagua hivyo basi niwaombe wananchi kujitokeza kwenye uandikishaji daftari la makazi lakini pia wajitokeze kwenye chaguzi hizi za serikali za mitaa kutumia haki yao ya msingi kabisa ya kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo"
"Lakini pia ni ukweli usiofichika serikali hii ya mheshimiwa Rais Samia imetekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa Nchi nzima hii ni ishara ya kuonyesha Chama cha mapinduzi kinasimamia kikamilifu serikali iliyopo madarakani".
"Alisema waziri Mkuu mstaafu Jonh Malecela ".
Amesema serikali ya awamu ya sita imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wake akisema miradi ya afya,maji, barabara na elimu imekuwa ikipatiwa fedha nyingi kitu ambacho kimeleta mapinduzi makubwa ya maendeleo kwa wananchi wakiwemo wananchi wa Jimbo la Same mashariki.
Hata hivyo uandikishaji daftari la makazi unatarajiwa kuanza tarehe 11-20 October na uchaguzi wa serikali za mitaa ukitarajiwa kufanyika tarehe 27 November mwaka huu huku wananchi wakiombwa kujitokeza kwenye uandikishaji huo na kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
0 Comments