Zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo Maisha yao yameunganishwa na bahari ya Hindi yanategemea uchumi wa bahari Katika, utalii usafirishaji na Uvuvi.
sambamba na hayo Taasisi ya Sea Sense imezindua Mradi wa USAID Heshimu bahari unaotekelezwa Wilaya ya Bagamoyo ukiwa na Malengo ya kuimarisha ustahimilivu wa kimazingira na uzalishaji wa Maeneo ya kiikolojia bahari.
Akizungumza Wakati wa ufunguzi wa Mradi wa USAID Heshimu bahari unaotekelezwa Bagamoyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Rashid Mchata amewapongeza Sea Sense Kwa Mradi ambao muhimu Kwani utasaidia Kuokoa mazao ya bahari na utaongeza juhudi za Pamoja Katika kutatua Changamoto zinazokabili Mazingira ya bahari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa sea Sense Gosbert Katunzi amesema
rasilimali za bahari zimekuwa zikipungua kwa Kasi kwasababu ya Uvuvi usioendelevu na Uvuvi haramu.
Aidha Meneja wa Mradi USAID Heshimu bahari Kutoka Sea Sense Lydia Mgimwa anaeleza namna Mradi huo ulivyoundwa na utakavyotekelezwa na wadau mbalimbali.
Mradi huu USAID Heshimu bahari utasaidia Wananchi wa Bagamoyo Katika kuboresha Hali ya Maisha Kwa kuondoa umasikini ,utasaidia kuondoa Hali ya umasikini ,na kutoa Elimu juu ya utunzaji wa bahari
0 Comments