Header Ads Widget

WADAU WA UCHAGUZI KASULU WATAKIWA KUZINGATIA 4R ZA RAIS SAMIA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Dk. Semistatus  Mashimba ametoa maelekezo kwa wadau  wa uchaguzi katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma  kutumia taratibu zinazoakisi 4R za Rais Samia Suluhu Hassan ili kuwezesha uchaguzi wa serikali za mitaa katika halmashauri hiyo kuwa huru, wa haki na shirikishi.

 

 Msimamizi huyo wa uchaguzi ametoa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye halmashauri hiyo    katika mkutano uliohusisha viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa dini,wazee maarufu,vyama vya wafugaji na wakulima,watendaji wa vijiji na kata pamoja na waandishi wa habari. 



 Dk. Mashimba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kasulu alisema kuwa ni takwa la kisheria lililomtaka kufanya hivyo  ili wananchi wapate maelezo siku 62 kabla ya tarehe ya uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa kwa wapiga kura pamoja na wagombea kupata taarifa zote kwa wakati na kwamba 4R za Raisi Samia Suluhu Hassan ndiyo nafasi yake kufanyiwa kazi kikamilifu.


Msimamizi huyo wa uchaguzi alisema kuwa kampeni katika uchaguzi huo zitaanza tarehe 20 hadi 26 Novemba 2024 na uchaguzi utafanyika  Novemba 27 mwaka huu ambapo amewaomba  vyama vya siasa,viongozi wa dini na wadau wote mliopo kwenye halmashauri hiyo kudumisha amani  na utulivu ili kuwezesha uchaguzi kufanyika bila changamoto yeyote.

 


Akizungumza katika mkutano huo  Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kasulu, Abdallah Kazikwa   ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Mkazi ambalo ni tofauti na zoezi lililopita la uandikishwaji katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili waweze kuitumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

 


Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Machifu Mkoa wa Kigoma,Abel Bussa ametoa rai kwa kila mwananchi mwenye sifa kujitokeza kugombea pamoja na kutoa ahadi ya kwenda kufundisha aliyojifunza  kwa wengine juu ya umuhimu wa kupiga

 

Mwisho.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI