NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Zaidi ya wachezaji 100 wa Golf kutoka mataifa mbalimbali Duniani wanatarajiwa kushindana septemba 21 na 22,2024 katika mashindano ya Diplomatic Golf kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa elimu ya sekondari kwa watoto walio katika mazingira magumu hapa nchini.
Akiongea na waandishi wahabari Septemba 20 Mratibu wa mashindano hayo Reinafrida Rwezauravalisema kuwa mashindano hayo ya 6 tangu kuanzishwa kwake yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Golf uliopo Usariver, Wilaya Arumeru ambapo wachezaji 132 wa jinsia na marika yote wamejisajili kushiriki mashindano hayo kati yao wapo wazee, vijana, wanawake na watoto.
"Mwaka huu tumekuwa wabunifu zaidi kwa kuhakikisha tunakidhi mahitaji yote ya washiriki wetu lakini sio kwamba wako kwenye ushindani bali ni sehemu ya kufurahia lengo likiwa ni kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu,"Alieleza.
" Pamoja na kwamba wanakuja kujifurahosha mwisho wa siku tunawapa wale washindi zawadi na mwisho wa siku wanawachangia watoto wanaoishi katika mazingira magumu," Alieleza.
Alifafanua kuwa katika kusaidia watoto hao kupata elimu kuna shule waliongia nayo makubaliano iliyopo mkoa Dar es salaam ambapo ili kuwapata watoto hao wanaanzia ngazi ya chini kulingana na utaratibu waliojiwekea.
Kwa upande wake Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus alisema kuwa benki hiyo ni mdao wa michezo hivyo wameweza kushirikiana na waandaaji wa mchezo huo kwa kutoa Tishet, kofia na Taulo 150 lengo likiwa kusaidia katika mchezo huo...
"Kama benki hii kwetu ni fursa kwa kuwa sehemu ya mashindano haya lakini pia tutapeleka wachezaji wa NMB kwani pia tunatambua kuwa michezo ni ajira na hii itachochea ukuaji wa mchezo huo hapa nchi," Alisema.
Aidha aliwata wanchi kuungana na benki hiyo katika mashindano hayo ili kuchochea mchezo wa Golf lakini kusaidia watoto wa tanzania walio katika mazingira magumu kupata elimu bora.
0 Comments