Header Ads Widget

MUNGANISHO WA MAWASILIANO KULETA AJIRA MPYA NA UPATIKANAJI WA MASOKO YA KIMATAIFA.

 


NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Katibu mkuu Wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Mohammed khamis Abdulla amesema kuwa kuongezeka kwa muunganisho wa mawasiliano kunaweza kuunda ajira mpya na tija,ikiwa ni pamoja kuwezesha upatikanaji wa masoko ya kimataifa hali itakayosaidia  kupunguza umaskini na ukosefu wa usawa.

Abdulla aliyasema hayo wakati akifunga mkutano wa Conect to Conect 2024 uliowakutanisha wataalamu na watendaji wa sekta ya mawasiliano wa tasisi za serikali,  binafsi na kutoka nchi mbalimbali uliofanyika kwa siku mbili mkoani Arusha, ambapo alisema kuwa  kumekuwa ishara ya azma yao ya pamoja ya kufikia kilele kipya katika sekta ya TEHAMA kwa kupata maarifa muhimu katika  mipango ya ukuaji wa siku zijazo na usaidizi unaohitajika kutoka kwenye mfumo.

Alisema kuwa kwa upande wa Tanzania uchumi wa Kidijitali umeleta  mageuzi ya athari za TEHAMA katika sekta mbalimbali nchini kwa kuangazia faida za kiuchumi kwani  vituo vya data katika ubadilishaji dijitali ilishughulikia masuala muhimu kama vile usalama, mamlaka ya data na utegemezi wa mitandao ya masafa marefu hivyo kuna umuhimu wa  kuendelea  kuharakisha ufikiaji na kupunguza vizuizi vya kuingia.

"Ajenda ya Umoja wa Afrika kufikia 2063 inasisitiza kuwa teknolojia za kidijitali ni muhimu kwa ajili ya kufikia mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, kwani zinawezesha utawala bora, kuimarisha utoaji wa huduma, na kuwawezesha wananchi kupata taarifa na fursa, kwahiyo muunganisho huu unaweza kuendeleza maendeleo endelevu na kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma kidijitali," Alisema.

Aidha alieleza kuwa katika mkutano huo wameweza kujadili uwezo wa kumudu wa ufikiaji wa vifaa vyenye nguvu za huduma za muunganisho kwa bei ya chini jambo ambalo ni muhimu katika kuunganisha watumiaji na biashara kwenye mfumo wa kidijitali hivyo tjmechungiza hifadhi za teknolojia zinazoibuka na mageuzi ya miundombinu ya kasi ya juu  na yenye uwezo wa juu.

 "Hii ni pamoja na kuwa na miundombinu Mahiri inayozingatia ufanisi, usalama na mamlaka ya taarifa ya miundombinu  na tumehitimisha kwa kupata jopo la  wawezeshaji vijijini litakalochunguza miundo bunifu ya biashara na teknolojia zinazowezesha kuwepo kwa uchumi na uwezeshaji katika maeneo ya vijijini,"Alieleza.


Kwa upande wake  mkurugenzi wa biashara kutoka shirika la mwasiliano Tanzania  (TTCl ) Vedastus Mwita alisema kuwa wamejadili ni jinsi gani wataweza kumlinda mtumiaji katika hatari ya udukuzi na uhalifu wa mtandaoni, kutoa huduma kwa usalama pamojana teknolojia mpya ambazo zinakuja ili kuongeza chachu ya mawasiliano duniani na nchini na kuongeza kasi na mawanda ya mawasiliano.

Alifafanua kuwa wataenda kuhakikisha wanayafanyia  kazi yote waliyoyajadili ili watanzania waweze kupata faida upelekewaji wa mawasiliano kwa kutoa huduma kwa bei nafuu na kuwawezesha kupata vifaa vya mawasiliano kwa gharama nafuu.

"Kama watoa huduma ni wakati muafaka wa  kuanza kutumia miundombinu kwa kushirikiana ili tusiongeze gharama kwankila mmoja kuweka miundombinu yake na kupunguza gharama ya kuweka mtandao kwa wananchi ili mwisho wa siku waweze kupata huduma kwa gharama nafuu," Alisema Mwita

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI