RC SERUKAMBA AVUTIWA NA UWEKEZAJI SHULE ZA REAL HOPE MAFINGA,ASEMA NI MATUNDA YA KAZI NZURI YA RAIS DR SAMIA
NA MATUKIO DAIMA APP,
MKUU wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba amepongeza jitihada Kuwa za Uwekezaji na ubora wa elimu katika shule za Real Hope Mafinga wilayani Mufindi kuwa ni matunda ya Uwekezaji unaofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza katika sekta ya elimu nchini kuwa Uwekezaji huo ni mkubwa na umeleta mapinduzi makubwa ya elimu nchini .
Uwekezaji huu mkubwa wa sekta ya elimu ni jitihada kubwa na tunapaswa kuendelea kumpongeza na kuunga mkono kwa wazazi kuhakikisha watoto wote wenye sifa ya kwenda shule wanakwenda shule .
Mkuu huyo wa mkoa ametoa pongezi hizi leo wakati wa Mahafali ya shule za msingi na Sekondari za Real Hope Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Alisema kuwa kupitia Uwekezaji wa serikali katika sekta ya elimu nchini pia wadau mbali mbali wakiwemo Real Hope Mafinga wameendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa kuwekeza katika sekta hiyo ya elimu .
"Nitumie nafasi hii kumpongeza mkurugenzi wa shule za Real Hope Dickson Mwipopo kwa Uwekezaji mkubwa na Bora katika sekta ya elimu "alisema Hata hivyo alipongeza uzalendo wa shule za Real Hope katika kuwatafutia ufadhili wa Masomo watoto wasio na Uwezo wa
kupata elimu hapa nchini.
Pia alisema ili elimu kuendelea kuwa Bora zaidi Suala la Uwekezaji zaidi kwenye nyenzo za kujifunzia na kufundishia kama maktaba za Kisasa ni jambo la msingi zaidi ambalo shule za Real Hope Mafinga limepania kufanya .
Ili Uwekezaji huo uwe Bora ni vema Suala la Walimu kuendelea kupata Mafunzo ya mara kwa mara kuendelea ili Walimu kuendelea kuwa Bora zaidi na wazazi kuendelea Kuchangua shule za Real Hope Mafinga Kwa ajili ya kupeleka watoto Wao .
Kuhusu wazazi mkuu huyo wa mkoa aliwataka wazazi kuendelea kupeleka watoto Wao shule kupata elimu .
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wanafunzi wanaotaraji kufanya mtihani wa kidato Cha nne mwaka huu na wale Waliofanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba kuendelea kujisomea zaidi na kuwa na ndoto za kufika mbali zaidi .
Akisoma risala ya shule hiyo kwa niaba ya uongozi wa shule mwalimu Geofrey Lukosi alisema kuwa shule hiyo ilianza mwaka 2016, huku ikiwa na jumla ya wanafunzi 41 ambapo wamekua wakiongezeka mwaka hadi mwaka na mpaka sasa wana jumla ya wanafunzi 301 na shule imeshatoa kidato cha nne mara tano na hii ya leo ni mara ya sita, ongezeko hili la wanafunzi limetokana na uboreshaji wa siku kwa siku katika nyanja za taaluma, nidhamu na miundombinu kwa ujumla.
Vile vile Ongezeko hilo la wanafunzi limepelekea fursa za ajira katika jamii inayotuzunguka ambapo wakati shule inaanza kulikuwa na jumla ya wafanyakazi 13 na sasa kuna jumla ya wafanyanyakazi 27 walimu na wasio walimu, hivyo Kuna walimu wa masomo yote kwa wastani mzuri kwa mwalimu na idadi ya vipindi kwa juma.
MIUNDOMBINU:
Alisema Shule ina miundombinu ya kujitosheleza kwa upande wa madarasa mabweni, maabara, vyoo na kumbi, kwa ajili ya watoto wetu, hivyo watoto wanapata mazingira mazuri ya kiufundishwaji na ujifunzaji.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shule za Real Hope Dickson Mwipopo akizungumza mipango ya shule hizo alisema lengo ni kuona shule hizo zinaendelea kufanya vizuri zaidi na ikiwezekana Kuongoza kimkoa na hata Kitaifa .
"Shule za Real Hope Mafinga ni miongoni mwa taasisi zinazojitahidi kuboresha elimu katika mkoa wa Iringa, Tanzania. Zinafahamika kwa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa ngazi za awali, msingi, na sekondari. Shule hizi zina mazingira mazuri ya kujifunza, ikiwa ni pamoja na madarasa ya kisasa, walimu wenye ujuzi, na vifaa vya kufundishia vya kutosha."alisema
Alisema shule hizo zinatilia mkazo nidhamu, maadili, na malezi ya kina kwa wanafunzi. Mbinu za kisasa za kufundisha, pamoja na ushirikiano kati ya wazazi na walimu, huchangia kuimarisha ufaulu wa wanafunzi na kuwasaidia kufikia malengo yao ya kitaaluma bila kusahau Kumcha Mungu kwa Kila mmoja kwa Imani yake .
Alisema kuwa Wazazi wanapaswa kusomesha watoto wao shule za Real Hope Mafinga kwa sababu ya ubora wa elimu unaotolewa, walimu wenye uzoefu, na mazingira bora ya kujifunzia. Shule hizi pia zinazingatia nidhamu na maadili, hivyo kuwasaidia watoto kukua kiakili na kimaadili. Mbinu za kisasa za kufundisha na vifaa vya kufundishia vilivyoboreshwa vinawawezesha wanafunzi kufaulu vizuri. Ushirikiano kati ya walimu na wazazi pia unachangia maendeleo ya mtoto, na kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata usikivu wa kutosha katika safari yake ya kielimu.
0 Comments